Home Kitaifa Makocha kuhusu wachezaji wa Mbeya City kuzidi uwanjani

Makocha kuhusu wachezaji wa Mbeya City kuzidi uwanjani

17720
0
SHARE

Kizaazaa kiliibuka kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga baada ya benchi la ufundi la Yanga kumfuata na kumlalamikia fourth official kwamba Mbeya City iliendelea kucheza na wachezaji 11 badala ya 10 kutokana na mchezaji wa timu hiyo kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 65.

Inasemekana: Mmoja wa wachezaji wa Mbeya City aliumia hivyo ikabidi afanyiwe huduma ya kwanza nje ya uwanja, kuokana na muda kuendelea kuyoyoma huku mchezaji huyo akiendelea kupatiwa tiba, bechi la ufundi likaamua kufanya mabadiliko kwa kumtoa mchezaji huyo na nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji mwingine.

Baada ya madaktari kumaliza kutoa huduma ya kwanza mchezaji akamuomba mwamuzi kurudi uwanjani na akaruhusiwa kwa hiyo akarejea uwanjani na kuifanya Mbeya City kuwa na wachezaji 10 badala ya 11.

Kocha wa Mbeya City Nswanzurwimo Ramadhani amesema mwamuzi ndio anaweza kujibu kuhusu jambo hilo.

“Hilo suala sio mimi natakiwa kukijibu, mtu yeyote akiingia uwanjani sheria inasema mwamuzi asimamishe mpira amtoe nje. Mimi sikuona mtu aliyeingia uwanjani, mwamuzi ndio anaweza kujibu hilo swali”-Nswanzurwimo, kocha mkuu Mbeya City.

Kocha msaidizi wa Yanga Shadack Nsajigwa baada ya mabadiliko kufanywa na Mbeya City, mchezaji aliyetakiwa kutoka hakutoka na aliyetakiwa kuingia akaingia hivyo kuifanya idadi ya wachezaji wa Mbeya City kuwa 11.

“Refa alimruhusu mchezaji aliyepata majeraha kurudi uwanjani wakati huo Mbeya City walishafanya mabadiliko aliyeumia akarudi uwanjani na aliyeingia kwa kuchukua nafasi yake wote wakaendelea kuwepo uwanjani”-Nsajigwa kocha msaidizi Yanga.

“Kwa hiyo Mbeya City wakaendelea kuwa 11 uwanjani badala ya kubaki 10 kama nitakuwa sahihi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here