Home Dauda TV Video-Yanga walivyotua Dar kutoka Ethiopia baada ya kufuzu makundi Caf

Video-Yanga walivyotua Dar kutoka Ethiopia baada ya kufuzu makundi Caf

7191
0
SHARE

Yanga imewasili salama Dar es  Salaam usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa kutoka Ethiopia ambako ilifanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuitoa Wolaitta Dicha kwa jumla ya magoli 2-1 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Aprili 7, 2018 jijini Dar es Salaam Yanga ilishinda 2-0 kisha ikapoteza 1-0 ugenini lakini imefanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa jumla.

Licha ya kuwasili ‘usiku wa manane’ baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo walikuwepo kuipokea timu yao ambayo iacheza hatua ya makundi kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2016.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here