Home Kimataifa Safari ya Wenger kutoka kwao kwenda Ufaransa kabla ya kuja Uingereza(Part 1)

Safari ya Wenger kutoka kwao kwenda Ufaransa kabla ya kuja Uingereza(Part 1)

10315
0
SHARE

Wenger anaondoka, hii sio mara ya kwanza lakini kwa Wenger kuondoka ama kuondolewa katika klabu. Pamoja na habari kwamba Wenger ametaka kuondoka Arsenal lakini ukweli ni kwamba Wenger anaonekana kulazimishwa.

Wenger aliazaliwa katika familia ya biashara mwaka 1949, familia yao walikuwa wakimiliki duka la vifaa vya magari huko Ufaransa, lakini b Wenger alianza kupenda soka akiwa mdogo na baba yake anadai mwanaye alijiunga katika soka akiwa na miaka 6 tu.

Wakati akiwa mtoto katika kijiji chao alijiunga na timu kwao iitwayo FC Duttlenheim, timu yao kama ilivyo timu za mtaani zingine haikuwa na kocha walikuwa wakicheza cheza tu, lakini baadae Arsene Wenger alianza kuifundisha timu hiyo huku akiwa mchezaji(kocha mchezaji).

Mwaka 1969 klabu ya Mutzig ilimuona Wenger na kujiunga nao lakini Wenger baadae aliona soka sio kitu chake sana , Wenger aliona ni bora ahamie katika kusimamia biashara za familia yao na kuanza kusoma chuo.

Akiwa katika biashara alianza kujifunza kuhusu mbinu za soka kwa kusoma vitabu vya soka kwenye muda wa ziada chuoni, na akaangalia zaidi soka la nchini Ujerumani Bundesliga, lakini naadae alijiunga na chuo cha Strasbourg ili kusoma masomo ya masuala ya uchumi na siasa ambako alipata degree.

Kama haufahamu tu ni kwamba Arsene Wenger ana diploma ya ukocha na mafunzo haya alihitimu mwaka 1981. Mwaka 1987 Wenger ndipo alianza kufundisha soka akiifundisha Nancy ya nchini Ufaransa.

Baada ya maisha magumu ndani ya Nancy baadae Wenger alijiunga katika klabu ya Monaco hii ikiwa 1987. Akiwa Monaco mwaka 1991 Wenger aliwapa kombe la Coupe de France lakini aliposhindwa kutetea kombe hilo akatimuliwa.

Wenger huyoo akaenda Japan, huku akifanikiwa kuifundisha Nagoya Grampus Eight ambapo walifanikiwa kushinda Emperor’s Cup na Jaoesse Super Cup na akaanza kukubalika sana nchini Japan na kupewa kocha bora wa msimu.

Ilikuwaje safari ya Japan? Wenger alikuwa mmoja kati ya jopo la FIFA ambalo lilikuwa likijadili kuhusu kombe la dunia 1994 katika mkutano uliofanyika Asia, na inasemekana hotuba yake kuhusu michuano hiyo iliwavuta wamiliki wa klabu ya Nagoya Grampus Eight kumtamani.

Ushauri kutoka kwa marafiki na familia ukamfanya Wenger ajiunge Nagoya mwaka December 1994. Wakati Wenger anajiunga na Nagoya walikuwa wako katika kiwango kibovu sana lakini akawafanya wakashinda michezo 17 kati ya 27 kabla ya August 1996 kutangaza kuachana nao.

Japan kwenda Epl ,mwaka 1996 Arsenal walimtimua kocha wao Bruce Rioch na kati ya watu waliokua wakipigiwa debe kuchukua nafasi yake alikuwa ni Johan Cruyff lakini baadaye waliamua kumpa mikoba ya timu kocha Arsene Wenger.

Patrick Viera na Remi Garde walitangulua Arsenal na waliposajiliwa tu ndipo tetesi za Wenger kuichuka Gunners zikawa kubwa na kweli baada ya kumaliza tu mkataba wake nchi Japan, Wenger akaichukua Arsenal.

Na tangu ajiunge na Arsenal hadi hii leo Wenger ameshinda michezo 473 kati ya michezo 823 aliyoitumikia klabu hiyo huku akifungwa michezo 151 na kwenda suluhu katika michezo 199.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here