Home Kitaifa Mtibwa yatangulia Arusha

Mtibwa yatangulia Arusha

7861
0
SHARE

Magoli mawili ya kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Hassan Dilunga yameipeleka fainali Mtibwa ya Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Stand United kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Dilunga amefunga magoli yote kipindi cha kwanza dakika ya 30 na 39 na kuihakikishia ushindi timu yake katika mchezo huo.

Mtibwa imetangulia arusha ambako utachezwa mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Juni 2, 2018.

Mtibwa itacheza dhidi ya mshindi wa nusu fainali kati ya Singida United na JKT Tanzania inayotarajiwa kuchezwa Jumatatu Aprili 23, 2018

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here