Home Kimataifa Manchester United, Mourinho na wengine wanasemaje kuhusu Wenger?

Manchester United, Mourinho na wengine wanasemaje kuhusu Wenger?

14958
0
SHARE

Moja kati ya nembo ya EPL inaondoka, hata mashabiki wa Arsenal baadhi wanataka Wenger aondoke lakini habari ya yeye kuondoka wanahisi kama kitu kimepungu katika maisha yao, salamu za kuondoka kwa Wenger zimeanza kutumwa.

“Hongera kwa miaka 22 ndani ya Arsenal, tunakutakia kila la kheri katika maisha yako na mechi zilizobako za msimu huu kasoro mchezo wetu ujao” hao ni Manchester United kupitia Twitter.

“Huwa nawatakia kila la kheri wapinzani wangu, naamini muda wake bado kustaafu katika soka, sisi kama Manchester United tunamtakia kila la kheri na tunapaswa kumuaga kwa heshima tutakapokutana” Jose Mourinho.

Rafael Benitez “nimekuwa nikiongea mambo mazuri kuhusu yeye kila wakati, nimekuwa nikizungumzia namna alivyo mshindi kwa miaka mingi, hapa tunamzungumzia moja kati ya makocha bora kuwahi kutokea katika soka.”

Cesc Fabregas moja kati ya nyota waliotengenezwa na Wenger ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe mreefu kwa kocha wake huyo wa zamani.

“Siwezi kusahau namna ambavyo amekuwa akiniongoza na kuniunga mkono. Alikuwa kocha ambaye alikuwa akiniamini sana, alikuwa kama baba yangu na alikuwa akinihamasisha kuwa bora zaidi ,hakika unastahili furaha na heshima kubwa duniani” Fabregas.

“Nimekuwa nikivutiwa sana na yeye, ana vitu vingi sana unapaswa kujifunza kutoka kwake. Hata kama hakuwa na matokeo ya kufurahisha lakini hilo ndio soka. Naamini siku moja nitaonana naye na kumuambia kuhusu yeye Jurgen Klopp.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here