Home Kitaifa Kocha wa Mtibwa afichua siri ya mafanikio

Kocha wa Mtibwa afichua siri ya mafanikio

8481
0
SHARE
Zubery Katwila (kushoto) kocha mkuu wa Mtibwa Sugar

Baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup, Mtibwa Sugar imefuzu kucheza fainali ya mashindano hayo na inasubiri kucheza dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Singida United na JKT Tanzania.

Kocha wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila ametaja siri ya timu yake kufanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Stand United pamoja na mashindano hayo kwa ujumla akiwa ameiwezesha timu yake kuingia hatua ya fainali.

“Tuliwatuliza vijana kwa sababu tulitoka kupoteza mchezo wa ligi (dhidi ya Kagera Sugar) tulikuwa tunaingia kwenye mechi ngumu ya nusu fainali kwa hiyo lazima uingie kwa utulivu, ukiangalia mechi ya kufungwa iliyopita unaweza kuchanganyikiwa ukajikuta unapoteza mchezo. Tuliwaambia watumie nguvu na akili ili tupate matokeo.”

“Safu yangu ya ulinzi imefanya kazi kubwa kutokana na hali ya uwanja kutubana, uwanja haukuwa rafiki kwa timu zote mbili kwa hiyo lazima niwapongeze watu wa ulinzi na mbele wakafunga.”

Katwila pia amezungumzia kuhusu kuhusu kuwapa nafasi vijana wengi kwenye kikosi chake kama Hassan Mganga, Kibwana Ally, Salum Kihimbwa na wengine.

Kwa sababu hawa ndiyo wanakuja kuchukua nafasi kwa sababu mtibwa kila mwaka tunachukuliwa wachezaji wanaingia wengine sasa usipowaamini vijana hawa huko baadae wote watakuwa wageni ndiyo maana tunawaingiza vijana kwenye nafasi ambazo wengine wameondoka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here