Home Kitaifa Kocha Stand United alia na uwanja

Kocha Stand United alia na uwanja

9090
0
SHARE

Safari ya Stand United kuwania ubingwa wa Azam Sports Federation Cup imekatishwa na kwenye uwanja wao wa Kambarage shinyanga baada ya Hasaan Dilunga kuifungia Mtibwa Sugar mabao wili kwenye mchezo wa nufu fainali na Stand kung’olewa kwa kufungwa 2-0.

Kocha wa Stand United Nianga Bwamazi amesema kufanya vibaya kwa timu yake kumesababishwa na ubovu wa uwanja kutokana na kujaa tope na maji.

“Uwanja haukuwa rafiki, ukiangalia magoli tuliyofungwa yametokana na makosa ya kutereza lakini hata sisi tulipata nafasi kama uwanja ungekuwa mzuri pengine matokeo yangekuwa mengine lakini uwanja umetuangusha kwa kiasi kikubwa.”

“Kipindi cha pili tulicheza mpira sana tukapata nafasi lakini kutokana na hali ya uwanja hatukuweza kuzimalizia vizuri. Timu pinzani tulikuwa tunaiheshimu lakini wameweza kupata magoli rahisi lakini kimchezo hatukucheza vibaya, wenzetu wamepata matokeo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here