Home Kimataifa Mnaosema “Lukaku mbovu” hamjui msemacho, soma hapa

Mnaosema “Lukaku mbovu” hamjui msemacho, soma hapa

10263
0
SHARE

Mpira ni takwimu, takwimu ndio zinaonesha kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mchezaji. Takwimu hizo ndio zinaonesha kwamba Romelu Lukaku mwaka huu ndio msimu wake bora zaidi Uingereza.

Kwanza Lukaku bao lake la jana kwa United limemfanya kuwa na mabao 27, Lukaku anakuwa amefunga mabao mengi zaidi katika msimu wake wa kwanza United kuliko washambuliaji wengine kama Rooney, Berbatov na Tevez.

Katika msimu wake wa kwanza Manchester United Tevez alifunga mabao 19, Wayne Rooney mabao 17, Dimitar Berbatov mabao 14, Andy Cole 12 lakini Lukaku hadi sasa ana 27 na mechi zinaendelea.

Achana na hilo lakini pia tangu msimu wa 2009/2010 hadi msimu huu 2017/2018, huu ndio msimu ambao Romelu Lukaku amefunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja, hajawahi kufikisha idadi hii ya mabao tangu ajiunge EPL.

Manchester United jana walishinda bao 2-0 dhidi ya Fc Bournamouth, na sasa United wanakuwa wamefunga jumla ya mabao 65 katika msimu huu, hii ni idadi kubwa zaidi tangu wafunge mabao 85 msimu 2012/2013.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here