Home Kimataifa Jay Z awaunganisha Romelu Lukaku na DJ Khaleed 

Jay Z awaunganisha Romelu Lukaku na DJ Khaleed 

10446
0
SHARE

Wakati Romelu Lukaku akifunga bao lake la 27 katika msimu huu usiku wa jana dhidi ya Fc Bournemouth alionekana akishangilia kwa kuunganisha vidole na kuweka umbo kama la pembe tatu.

Ushangiliaji ule mara nyingi hutumiwa na msanii Jay Z akiwa katika maonesho yake, ile ni alama ambayo huwakilisha nembo ya mwanamuziki Jay Z. Mashabiki wengi walianza kujiuliza kwanini Lukaku alifanya vile.

Baasi ishu iko hivi, Romelu Lukaku kwa sasa yuko chini ya Jay Z. Tangu mwezi uliopita Lukaku alisaini mkataba na Roc Nation lakini bado walikuwa hawajaanza kufanya kazi rasmi hadi mwezi huu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter na Instagram Lukaku ameandika kwamba kwa sasa ni mwanafamilia wa Roc Nation ambapo kuanzia sasa kazi zake zote na masuala yake ya kibiashara yatasimamiwa na Roc Nation.

Roc Nation walikuwa wamejikita zaidi katika masuala ya muziki ambapo wamekuwa wakisimamia wasanii wakubwa ikiwemo Dj Khaleed na sasa wamehamia katika soka na kumsaini Lukaku huku Marcus Rashford naye akitajwa kuwa njiani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here