Home Kimataifa Unadhani umeshaona yote kuhusu VAR? hili litakustaajabisha zaidi limetokea Ujerumani

Unadhani umeshaona yote kuhusu VAR? hili litakustaajabisha zaidi limetokea Ujerumani

11720
0
SHARE

VAR bado ni habari kubwa katika ulimwengu wa soka, teknolojia hii imekuwa ikipigwa vita sana katika sehemu mbalimbali na wachambuzi wengi kuishambulia kwamba imeharibu utamu katika soka.

Sasa nchini Ujerumani kumetokea tukio la ajabu zaidi kuhusu VAR, hii imetokeoa katika mchezo kati ya Mainz na Freiburg, mchezo huu ulikuwa wa timu mbili ambazo zote zinapambana kutoshuka daraja.

Ilikuwa wakati wa mapumziko ambapo wakati wachezaji wakienda kupumzika muamuzi Guido Winkmann aliamua kuwaita uwanjani baada ya muamuzi aliyekuwa akiangalia VAR Bibiana Steinhaus kumuita muamuzi huyo na kumuonesha tukio la mpira ulioguswa na mkono.

Baada ya kujiridhisha kwamba mchezaji wa Friburg Marc Oliver Kempf  aliunawa mpira huo ndipo Winkmann aliwaita wachezaji kurudi uwanjani na kuwapa Mainz zawadi ya tuta ambalo walifunga.

Kocha wa Freiburg Christian Streich amesema hakuwa anaelewa nini kinaendelea na aliwaambia wachezaji wake wasirudi uwanjani baada ya refa kuwaita japo baadae walitoka baada ya waamuzi wa ziada kuwaleza nini kinachotokea.

Jochen Saier ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa Freiburg amehoji penati hiyo haswa itakuwa imefungwa dakika ya ngapi, huku akihoji kwamba anaelewa kipyenga cha halftime kikipigwa ndio muda umeshapita hivyo anashangazwa na kilichotokea.

Mchezo huo mbaya zaidi umepigwa siku ya Jumatatu siku ambayo mashabiki wengi Bundesliga wameikataa, na tukio la muamuzi Winkmann liliwafanya mashabiki kutupa toilets paper nyingi uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here