Home Kitaifa Tetesi kocha wa Mbao anaondoka “Hatuwezi kumzuia kwenda anapoona panamfaa”

Tetesi kocha wa Mbao anaondoka “Hatuwezi kumzuia kwenda anapoona panamfaa”

11345
0
SHARE

Uongozi wa Mbao umesema bado wana mkataba na kocha Etiene Ndayiragije, endapo atapata sehemu nyingine itakayokuwa bora zaidi kwake hawatamzuia kwa sababu mpira ni biashara na maisha ya mtu.

Mwenyekiti wa Mbao Solly Njashi amesema bado wanamkataba na Etiene lakini endapo kuna timu itahitaji huduma ya kocha huyo wapo tayari kumwachia.

“Bado tunamkataba na Ndayiragije hatujauvunja na ikitokea mkataba umevunjwa tupo tayari kwa lolote kwa sababu huwezi kumzuia mtu kwenda mahali anapoona panamfaa na patamlipa zaidi.”

“Mwisho wa siku mpira ni biashara na ni maisha ya mtu kwa hiyo kama kuna mahali pengine pazuri hatuna ubaya juu la hilo lakini bado tunamkataba ba Ndayiragije.”Naendelea vizuri kwenye ligi ya Tanzania kama nikiendelea vizuri naweza kufanyanvizuri zaidi na kuisaidia timu yangu Singida United.

Ndayiragije amekuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa watetezi wa VPL Yanga baada ya kocha wao mkuu George Lwandamina kuondoka na kuacha timu bila kocha mkuu. Zipo pia taarifa zinazodai kwamba Ndayiragije atajiunga na Singida United kufuatia Hans van Pluijm kutajwa kutakiwa na Azam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here