Home Kitaifa Shaffih Dauda kuhusu penati na kadi nyekundu Simba vs Prisons

Shaffih Dauda kuhusu penati na kadi nyekundu Simba vs Prisons

15336
0
SHARE

Uamuzi wa mwamuzi Shomary Lawi kutoka Kigoma kutoa adhabu ya penati wakati wa mchezo wa ligi kati ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons umezua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii, wadau wengi  wanabishana kama uamuzi huo ulikuwa halali au la.

Wanaokubali kwamba mwamuzi alikuwa sahihi wana kigezo chao kuwa  beki wa Prisons Jumanne El Fadhili alimwangusha Bocco kwa kufanyia madhambi Bocco akiwa nyuma huku yeye akiwa beki wa mwishol akini wanaopingana na maamuzi ya refa wanasema beki aliucheza mpira kabla ya John Bocco kunguka.

Kwa upande wa Shaffih Dauda yeye ameunga mkono maamuzi ya refa kwamba Prisons walistahili kuadhibiwa kwa penati na ametoa sababu zake kwa nini tukio lile lilistahili kuwa penati.

“Pamoja na kuucheza mpira inategemea pia maamuzi ya mwamuzi alikuwa wapi na ataamua nini bahati mbaya yule beki alijaribu kuucheza mpira akiwa nyuma ya Bocco, licha ya kujaribu kuucheza mpira lakini bado alimgusa Bocco.”

“Tukio la penati ya Bocco halina tofauti sana na lile lililotokea katikati ya wiki iliyopita kwenye mchezo wa Uefa Champions League kati ya Real Madrid na Juventus penati iliyowahusisha Benatia na Vasquez ambayo ilizua mjadala kwamba Benatia alicheza mpira na hakumgusa Vasquez.”

“Kwenye eneo la penati box beki anahitaji kuwa makini sana kwa sababu mara nyingi mshambuliaji anapokuwa na mpira anapewa advantage kwa sababu yeye anakuwa kwenye nafasi ya kufunga kwa hiyo lolote linalotokea kujaribu kumzuia mshambuliaji kufunga mwamuzi anatoa hukumu.”

Kuhusu mchezaji wa Prisons Jumanne El Fadhili kutolewa kwa kadi nyekundu Duda amesema, alistahili kuoneshwa kadi nyekundu kwa sababu tayari alikuwa na kadi ya njano, kosa alilofanya (kumwangusha Bocco kwenye eneo la penati) lilistahili kadi ya njano na kwakuwa alikuwa na njano aliyopata mapema kadi nyekundu ilikuwa haikwepeki.

“Sheria ya kumwonesha kadi nyekundu mchezaji aliyefanya madhambi ndani ya penati box ilibadilishwa, zamani ilikuwa kwamba mchezaji akifanya kosa ndani ya eneo lake la hatari mwamuzi anatoa adhabu ya penati na mchezaji aliyefanya kosa anaoneshwa kadi nyekundu lakini baadaye ikafanyiwa marekebisho kwa sababu ilikuwa inatoa adhabu mbili kwa wakati mmoja (panati na kadi nyekundu).”

“Kilichotokea kwa mchezaji wa Tanzania Prisons kuoneshwa kadi nyekundu ni kwa sababu tayari alikuwa na kadi ya njano kwa hiyo alioneshwa kadi ya pili ya njano ambayo moja kwa moja inamhukumu kuoneshwa kadi nyekundu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here