Home Kitaifa Okwi, Bocco, wakataa kiatu cha ufungaji bora 

Okwi, Bocco, wakataa kiatu cha ufungaji bora 

10697
0
SHARE

Emanuel Okwi amefikisha magoli 19 ina John Bocco amefikisha magoli 14 baada ya kila mmoja kufunga goli moja kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Jumatatu Aprili 16, 2018 kwenye uwanja wa taifa.

Ukiwauliza kuhusu kiatu cha ufungaji bora msimu huu kila mmoja anakikataa si Bocco wala Okwi, wote wanasema malengo yao ni kuisaidia Simba ifanye vizuri na kushinda kombe la VPL mambo ya ufungaji bora yatafuata baadaye.

“Mimi nacheza kwa ajili ya timu, nafunga na nitaendelea kufunga ili timu yangu ipate pointi tatu mwisho wa msimu Mungu ndiyo ataamua”-amesema nahodha wa Simba John Bocco ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa VPL akiwa na magoli 19.

Kwa upande wa Okwi ambaye ndio anaongoza orodha ya wafungaji wa VPL msimu huu, kuisaidia Simba kufanya vizuri ni jambo zuri zaidi ya yeye kuwa mfungaji bora.

“Naangalia zaidi kuisaidia timu yangu kupata pointi tatu na nashukuru tumepata pointi tatu na kuendelea kuongoza ligi hivyo ni vizuri zaidi kuliko mimi kuwa mfungaji bora.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here