Home Uncategorized Taarifa mbali mbali majuu

Taarifa mbali mbali majuu

9047
0
SHARE

Na Daniel s Fute

Zidane Atimiza Karne Ya Ushindi Akiwa Na Real Madrid

KOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane, usiku wa jana katika mchezo wa Ligi kuu ya Hispania ameweza kuweka rekodi yake ya kushinda michezo 100 katika mashindano yote akiwa na Real Madrid.

Zidane mbaye alitengeneza rekodi hiyo katika mchezo wa jana dhidi ya Malaga, ambapo Madrid waliweza kuishinda Malaga bao 2-1.

Mabao hayo yalifungwa na Isco aliyefunga kwa faulo pamoja na Casemiro, Isco ambaye alishawahi kuichezea Malaga kabla ya kujiunga na Madrid.

Mpaka sasa Zidane ameiongoza Real Madrid kwa misimu mitatu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na tayari ameshinda vikombe hivyo mara mbili mfululizo akiwa kocha wa klabu hiyo.

Ushindi huo wa 100 kwa Zidane unamfanya kuwa kocha mwandamizi kuwahi kutokea katika ardhi ya Ufaransa katika kipindi kifupi akiwa kama kocha.

KOMBE LA DUNIA (2018)

Golikipa Wa Misri Kukosa Fainali Za Kombe la Dunia

TIMU ya taifa ya Misri ipo katika pigo zito baada ya kupokea taarifa kwamba Golikipa wao Ahmed El Shenawy, ataweza kupoteza Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kupatikana na jeraha.

Daktari wa timu ya taifa Misri Mohamed Abu El Ela, amethibitisha taarifa hiyo na kusema kwamba golikipa huyo amepata jeraha la goti katika mechi ya ligi kuu Misri dhidi ya Al Ittihad.

“El Shenawy hawezi kucheza katika Fainali za Kombe la Dunia, baada kupatikana na jeraha katika goti,” alisema Abu El Ela.

El Shenawy,mwenye miaka 26, alikuwa sehemu muhimu ya kocha mkuu wa Misri Hector Cuper katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu lakini baada ya taarifa hii ni pigo zito kwa wachezaji pamoja na nchi kwa ujumla.

“Ninataka kumshukuru Allah kwa kila kitu kilichotokea, hii ndiyo hatima yangu na mimi nimekubaliana nayo,” El Shenawy aliandika katika twitter.

Hivyo golikipa huyu wa Zamalek hatukuwa katika kikosi cha Misri kitakacho kwenda Urusi kwenye Fainali hizo.

Daniel S.Fute

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here