Home Kitaifa Okwi, Bocco ni mwendo wa rekodi VPL

Okwi, Bocco ni mwendo wa rekodi VPL

8060
0
SHARE

Washambuliaji wa Simba John Bocco na Emanuel Okwi kila mmoja amefikia rekodi baada ya wawili hao kufunga kwenye mhezo wa ligi na kuisaidia timu yao kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Bocco alifunga goli la kwanza kwa kumalizia mpira uliopigwa na Erasto Nyoni ukagonga mwamba Bocco akafunga kwa kichwa. Bocco amefikisha magoli 14 na kufikia magoli ya Simon Msuva na Abdulrahman Mussa waliokuwa wafungaji bora wa msimu uliopita (2016/17).

Okwi amefunga kwa mkwaju wa penati baada ya Bocco kuangushwa kwenye penati box. Goli hilo ni la 19 kwa Okwi kwenye ligi msimu huu na kumfanya afikie idadi ya mganda mwenzake Hamisi Kiiza ndani ya Simba. Lakini Okwi pia ameifikia rekodi iliyoiwekwa na Amis Tambwe wakati yupo Simba na Bocco wakati yupo Azam kufikisha magoli 19 kwa msimu mmoja.

Okwi alianza kuivunja rekodi ya Simon Msuva na Abdulrahman Mussa ambao walikuwa wafungaji bora 2016/17 kwa kufunga magoli 14.

Hakuishia hapo, akavunja rekodi ya Kipre Tchechez aliyekuwa mshambuliaji wa Azam na Msuva kwa mara ya pili. Tchetche (Azam) mabao 17 2012/13, Msuva (Yanga) mabao 17 2014/15.

Amezivunja pia rekodi ya Boniface Ambani (Yanga) 2008/09 mabao 18, Musa Mgosi (Simba) 2009/10 mabao 18 na Mrisho Ngasa (Azam) 2010/11 mabao 18.

Okwi anaitafuta rekodi ya Abdallah Juma mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar ambaye alikuwa mfungaji mwaka 2006 kwa kufunga magoli 20 na Amis Tambwe mungaji bora 2015/16 ambapo alifunga magoli 21 akiwa Yanga.

Kwa pamoja Bocco na Okwi wamefikisha magoli 33 msimu huu huku zikiwa zimebaki mechi sita kwenye ligi.

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 58 baada ya kucheza mechi 24 za ligi wakati Yanga ikiendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 47, tofauti ya pointi 11lakini Yanga imecheza mechi 22.

Simba inaendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here