Home Kimataifa Serengeti Boys yaanza kwa sare yawaza ubingwa CECAFA

Serengeti Boys yaanza kwa sare yawaza ubingwa CECAFA

7648
0
SHARE

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imetoka sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mashindano ya CECAFA iliyoanza leo Aprili 15, 2018 nchini Burundi.

Kocha wa Serengeti Boys Oscar Mirambo amesema sio jambo baya kuanza  na pointi moja lakini lengo lao ni kucheza fainali ya mashindano hayo.

“Kuanza na pointi moja sio jambo baya watazamaji wote wanajua umefungwa goli la aina gani lakini sisi kama benhi la ufundi hatuna jukumu la kuzungumzia maamuzi isipokuwa tunaangalia ni kwa namna gani tunaweza kuboresha kile ambacho tuponacho na kufikia malengo kama timu.”

Mpaka tunaporudi kutoka Burundi ni lazima tucheze michezo mitano kwa maaba ya kwamba michezo mitatu ya hatua ya makundi, lazima pia tucheze mchezo wa nusu fainali na fainali ili vijana wetu wapate uzoefu.”

“Lengo tulilonalo ni kuhakikisha mwaka 2019 kwenye fainali za AFCON tunakuwa na timu ambayo itaweza kuleta faraja kwa watanzania.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here