Home Kitaifa Prisons yatamba kuisimamisha Simba “Hali ya hewa inaruhusu”

Prisons yatamba kuisimamisha Simba “Hali ya hewa inaruhusu”

10740
0
SHARE

Maafande wa Tanzania Prisons wamesema kesho wananafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi yao ya ligi dhidi ya Simba itakayochezwa uwanja wa taifa na kiburi chao kinatokana na hali ya hewa ya Dar kwa sasa kuwa rafiki kwoa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Meneja wa Tanzania Prisons Havitishi Abdallah amesema kesho moto utawaka uwanja wa taifa kuanzania saa 10:00 jioni.

“Tunataka tuwaambie Simba hii ni Prisons wasitufananishe na timu nyingine, sisi tutawafanyia kitu kibaya waamini hivyo kwa sababu tupo vizuri sana na hii hali ya hewatunapenda iwe hivihivi kwa sabbau tukikutana hali yetu ya hewa kama hii inakuwa burudani.”

“Hatuiogopi Simba ni kama timu nyingine tulizokutana nazo ni kweli wana jina kubwa na tuna waheshimu wapo juu lakini hiyo haitutishi, wana mwalimu mzuri na sisi tuna mwalimu mzuri ndiyo maana najiamini.”

Prisons itawakosa wachezaji wake watatu katika mchezo wao dhidi ya Simba, Laurent Mpalile, Kassim na Sabianka ambao wana matatizo, wachezaji wengine wapo vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here