Home Kitaifa Matola apania kuivunja rekodi ya Simba

Matola apania kuivunja rekodi ya Simba

9568
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Lipuli Selemani Matola amesema ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Singida United ni matokeo mazuri kwa Lipuli wakati wanaisubiri Simba kuivunjia rekodi ya kutofungwa kwenye ligi msimu huu.

“Mwisho wa mchezo huu ndiyo mwanzo wa mchezo mwingine, tutajipanga kwa ajili ya Simba tunajua mechi ijayo ni dhidi ya Simba timu ambayo haijafungwa kwenye ligi sijui kama inaweza kupoteza mechi yake kesho (Simba vs Tanzania Prisons) lakini sisi tunataka kuwa timu ya kwanza kuifunga Simba.”

Matola pia ameelezea kuhusu mchezo wao dhidi ya Singida United ulivyokua na ushindi walioupata kwenye uwanja wao wa nyumbani Samora, Iringa.

“Mechi ilikuwa ngumu sana kwa sababu ukiangalia Singida United ni miongoni mwa timungumu kwenye ligi ni timu ambayo imewekeza lakini nawapongeza wachezaji wangu kwa sabbau wamefanya kitu ambacho tumewatuma na kila mwana Iringa alitaka wakifanye.”

Malimi Busungu ameendeleza matokeo yasiyo pendeza kwa Singida United baada ya kufunga goli pekee la Lipuli na kuisaidia kupata ushindi wa goli pointi tatu katika mchezo huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here