Home Kitaifa Matokeo yamuumiza kocha Mbao

Matokeo yamuumiza kocha Mbao

7436
0
SHARE

Mbao imeshindwa kupata ushindi mbele ya Majimaji kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba baada ya kutoka sare ya kufungana 2-2.

Magoli ya Mbao yamefungwa na Boniphace Maganga dakika ya 59 na 63 huku magoli ya Majimaji yakifungwa na Marcel Kaheza ambaye alifunga dakika ya 81 na 90.

Kocha wa Mbao Novatus Furgence amesema ameumizwa na magoli ya kusawazisha ya Majimaji dakika za mwisho kwa sababu aliamini timu yake itashinda mchezo huo.

“Ni matokeo ambayo yameniumiza, kimsingi ni mechi tulikuwa tumeishika na tulikua tunaongoza 2-0 lakini vitu kama hivi huwa vinatokea uwanjani. Mpango wangu ulikuwa kushinda lakini hainikatishi tama, tunarudi kufanya mazoezi kwa ajili ya mechi zijazo lakini kikubwa tutafanya masahihisho kwa yale yaliyojitokeza.

“Haya ni matokeo ambayo yamemvunja nguvu kila mtu kwa sababu tulistahili kushinda lakini kukosa umakini  ndani ya dakika 90 ndiyo kumesababisha haya lakini ni vitu ambavyo tutaviongelea kuwa makini kwa dakika 90.”

Kwa upande wa Majimaji wanarudi Songea kwa ajili ya kujipanga kuona namna gani wanaweza kuepuka kushuka daraja na kubaki ligi kuu katika mechi zao zijazo.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kupambana kwa dakika zote 90 kuona kwamba hatupotezi mchezo wa leo, tulipanga kushinda lakini katika mchezo kama huu ambao ulikuwa na tension kubwa wakati mwingine game plan inapotea kwa hiyo kinachobaki ni wachezaji kujituma wenyewe ili kupata matokeo”-amesema kocha msaidizi wa Majimaji Habib Kondo.

“Hadi ligi itakapomalizika ndio tutajua kama tumebaki ligi kuu au tunashuka lakini kwa sasa bado kuna mechi nyingi  na sisi tunamatumaini ya kubaki kwenye ligi. Mashabiki wote wa Songea wasisononeke watuunge mkono katika mechi zilizobaki.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here