Home Kitaifa Masoud Djuma awazodoa mashabiki Simba, Yanga

Masoud Djuma awazodoa mashabiki Simba, Yanga

15277
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma ametaja vitu ambavyo amevibadilisha kwa muda mfupi tangu amejiunga na klabu hiyo, kocha huyo pia ametaja baadhi ya vitu ambavyo hapendi kwenye soka la Tanzania.

Akizungumza na Prisca Kishamba kocha huyo amesema miongoni mwa vitu alivyojitahidi kuviweka sawa ni maelewano kati ya benchi la ufundi na wachezaji kitu ambacho kilikuwa ni changamoto kipindi anafika katika klabu hiyo.

“Kwa kipindi kifupi ambacho nimekuwa Simba nimejitahidi kuweka maelewano kati ya wachezaji na benchi la ufundi hiki kitu hakikuwa sawa kidogo, kitu kingine ilikuwa ni kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza kitu cha tatu ilikuwa ni kuipa umuhimu ligi miaka mingi kabla mimi sijaja Simba haijapata ubingwa lakini kwa sasa Mungu ametusaidia japo hatuko mbali na wapinzani lakini bado Simba ipo juu.”

Kitu cha nne ni mashabiki, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji kila mtu afanye kazi yake bila kukata mtu kutoa maoni yake lakini isiwe kila unapotoa maoni ni lazima yafanyiwe kazi kama unavyotaka jambo hili nadhani linaifanya Simba ifanye vizuri.

“Kitu kilichonivutia Tanzania nimashabiki, nimefundisha Rayon Sports timu ambayo ina mashabiki wengi lakini hapa watu wote mjini, mitaani, wanazungumzia mpira, watu wanapenda sana mpira sikuwa nategemea hiki kitu. Inasababisha uwe makini kwa kila mechi.”

“Nafurahi kupata support kutoka kwa watu, wakati mwingine unapita mjini unaitwa na mtu hata humfahamu kitu kama hicho kinakupa nguvu. Unafanya kazi unafurahi, Tanzania nipo kama nyumbani licha kwamba ndiyo mara ya kwanza nimekuja kufundisha hapa.”

Kwa upande wa soka la Tanzania kuna vitu vipya ambavyo amekutana navyo ambavyo vinaweza kuifanya ligi na mpira wa Tanzania kuwa bora zaidi lakini hakuacha kukosoa utamaduni wa vilabu vya Simba na Yanga kuzomeana na kushangilia timu ngeni pale ambapo moja ya timu hizo zinapocheza mechi za kimataifa.

“Napenda sana upinzani lakini wakati mwingine uwe na kikomo, kwa mfano Yanga na Simba zinapokuwa zinacheza mashindano ya kimataifa halafu unakuta mashabiki wa Simba wanaizomea Yanga au mashabiki wa Yanga wanazomea Simba wanasahau kwamba hizo timu mbili ndio zitaifanya Tanzania ifike mbali. Mtanzania unamzoemea mwenzako unashangilia mtu anaetoka nje unataka nini?

“Kwa mfano Simba ikifanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ikafika hatua ya makundi ya kombe la vilabu bingwa Afrika msimu unaofuata timu zitaongezeka kutoka Tanzania kushiriki mashindano ya kimataifa na ndiyo nchi inajulikana. Sasa kwa mfano umemzomea mwenzano akapaniki timu zote zikatoka mnabaki kuzomeana wenyewe.”

“Ninachokiona ni kwamba timu ya Tanzania ikicheza mashindano ya kimataifa mashabiki wote waiunge mkono hata timu ya nje ikija inakuta watu wote ni kitu kimoja. Nakumbuka tulivyoenda Misri tulizomewa mwanzo hadi mwisho wa mechi lakini benchi la ufundi lilikuwa sawa, viongozi, ubalozi wa Tanzania na mashabiki wachache tuliowakuta kule. Yangekuwa mambo kama ya Simba na Yanga  tungepata support ya wenyeji tungeitoa   Al Masry lakini wenzetu walikuwa na support kubwa ya mashabiki. Hiki kitu kibadilike Tanzania kitasaidia sana.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here