Home Kimataifa Manchester City bingwa mpya EPL 2017/2018

Manchester City bingwa mpya EPL 2017/2018

9726
0
SHARE

Katika misimu yake tisa kama kocha katika ligi kuu mbali mbali Pep Gurdiola amechukua ubingwa mara 7 baada ya hii leo kutangazwa rasmi kuwa bingwa wa EPL, mara mbili pekee ambazo Pep amekosa ubingwa ni 2011/2012 na 2016/2017.

Kwa ubingwa huu ambao Manchester City wametwaa sasa kocha Pep Gurdiola anakuwa kocha wa kwanza kutoka nchini Hispania kuwahi kushinda taji la ligi kuu ya nchini Uingereza.

Kipigo cha United kutoka kwa WestBromich hii leo kinawafanya United kutoifikia City kwa idadi ya alama hata wakishinda mechi zao zote zilizobaki, huu ni ubingwa wao wa 3 wa Premier League.

Hii ni mara ya kwanza kwa kocha Jose Mourinho kushindwa kuchukua ubingwa katika msimu wake wa pili wa ligi tangu aanze kufundisha soka katika ligi kubwa barani Ulaya.

Kabla ya mchezo kati ya United na WestBromich kulikuwa na mchezo kati ya Newcastle na Arsenal ambapo Arsenal walipoteza kwa bao 2-1 na hii ikiwa mara ya kwanza kwao kupoteza mechi 5 mfululizo ugenini tangu 1984.

Hadi baada ya mchezo wa leo, Arsenal wanakuwa wameruhusu mabao mengi (45), hii ikiwa ni idadi ya bao moja zaidi ya idadi ya mabao waliyoruhusu kwa msimu mzima wa mwaka 2016/2017.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here