Home Kitaifa Juma Abdul ametaja kinachokwamisha wachezaji wa Tanzania kwenda Ulaya

Juma Abdul ametaja kinachokwamisha wachezaji wa Tanzania kwenda Ulaya

8752
0
SHARE

Ndoto ya wachezaji wengi ni kucheza Simba na Yanga na baada ya hapo ndipo inaanza mipango ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Juma Abdul ameshacheza nchini kwa kiwango cha juu akiwa na klabu ya Yanga na kufanikiwa kuchaguliwa mchezaji bora wa ligi kuu Tnzania bara.

“Nawaza sana kuchezaja nje ya Tanzania na sio mimi pekeyangu, kuna wachezaji wengi ambao wana vipaji vya kucheza nje lakini changamoto imekuwa nafasi au mawakala wetu kuwachukuwa wachezaji kuwapeleka sehemu wafanye majaribio kuona kama wanaweza kufanikiwa. Wachezaji wenzetu wa Afrika Magharibi wanaamini kile wanachokiamini mchezaji anaweza kuwa hana hata kipaji lakini anaamini nikifika sehemu fulani nikifanya kazi nitafanikiwa”-Juma Abdul wakati anazungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’.

“Kinachotukwamisha sisi waliotutangulia mwanzo kabisa hawakuweka njia nzuri mimi naamini hata Nigeria sasa hivi wachezaji wengi wanatoka kwenda kucheza Ulaya siyo kwamba ni wachezaji hatari lakini ni njia ambayo imewekwa na waliowatangulia kwa hiyo sasa hivi ni rahisi kwa wakala kwenda Nigeria kuangalia wachezaji na akifika kweli anakutana nao ambao anajua wakifundishwa baadhi ya vitu wanakuwa wachezaji wazuri.”

“Tunachokosa sisi ni watu wa kutushika mkono kutupeleka sehemu fulani lakini  kwa mfano akipatikana mtu akaamua kunishika mkono mimi, Hassan Kessy, Shomari Kapombe au Ibrahim Ajib naamini tunaweza kufanikiwa. Mfano mzuri ni Msuva sio kwamba ile timu ilimuona lakini kuna mtu alimwambia nakupeleka sehemu fulani naamini utafanikiwa kweli Msuva kafanya kazi amefanikiwa.”

Ameongelea pia kuhusu watu wakahoji kwamba Juma Abdul amecheza pamoja na Msuva katika klabu Yanga je amewahi kuzungumza na Msuva ambaye kwa sasa anacheza Morocco ili kuona ni kwa namna gani anaweza akamsaidia?

“Huwezi kusema sasa hivi Msuva anaweza kutusaidia sisi kwa sababu yeye mwenyewe bado anatafuta njia ya kufika sehemu, kwa mfano Samatta ametoka Tanzania akaenda Congo leo yupo Ubelgiji ni rahisi Samatta kuzungumza na watu wa Mazembe kuwambia kuna kijana mzuri yupo sehemu fulani mfuatilieni anaweza kuwasaidia hizo ndiyo nja ambazo mchezaji anaweza kuwasaidia wengine lakini sio yeye ndio kwanza anajenga jina lake aanze kusaidia wengine.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here