Home Kitaifa Azam yaomba ‘poo’ bodi ya ligi

Azam yaomba ‘poo’ bodi ya ligi

8167
0
SHARE

Wakati ratiba ya ligi kuu Tnzania bara ikionesha leo Jumapili Aprili 15, 2018 kutakuwa na mchezo kati ya Azam dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Azam Complex, Azam wameilalamikia bodi ya ligi juu ya ratiba inavyowabana kwa kucheza mechi mbili tofauti ndani ya muda mfupi.

April 13, 2018 Azam ilicheza ugenini dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Mabatini, Mlandizi na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa 2-0. Awali mchezo huo ulikuwa ulipangwa kucheza Aprili 12, 2018 lakini ulisogezwa mbele kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo na kuufanya uwanja usiruhusu mechi kuchezwa.

Afisa habari wa Azam Jafar Idd amesema wameandika barua kwenda bodi ya ligi kuomba mchezo wao dhidi ya Njombe Mji usogezwe mbele ili kutoa fursa kwa wachezaji kupumzika kwa mujibu wa kanuni za ligi.

“Kanuni zinataka timu icheze moja hadi nyingine kwa tofauti ya saa 72, sisi tumecheza Ruvu Shooting Ijumaa Aprili 13 tunatakiwa kucheza mechi nyingine Jumapili Aprili 15 kitu ambacho kipo nje ya kanuni. Kwa maana hiyo wachezaji watakuwa wamepumzika kwa saa 48 tu tangu tulivyocheza na Ruvu Shooting.”

Jafar amesema timu imeendelea na maandalizi Jumamosi mara baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting na maandalizi hayo ni ni kuelekea mechi yao dhidi ya Njombe Mji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here