Home Kimataifa Arsenal kuweka rekodi yao mbovu ugenini ya 1925 au kuendeleza utemi kwa...

Arsenal kuweka rekodi yao mbovu ugenini ya 1925 au kuendeleza utemi kwa Newcastle

6004
0
SHARE

Pierre-Emerick Aubameyang anaweza kuwa mchezaji wa kwanza wa Araenal kufunga mabao katika mechi 5 mfululizo za Arsenal tangu Olivier Giroud afanye hivyo wakati yupo Arsenal mwaka 2015.

Tayari Arsenal wamepoteza michezo 4 mfululizo ugenini,mara ya mwisho wanapoteza mechi 5 mfululizo ugenini ilikuwa 1984/1985 na mwaka huo baada ya mechi hizo walizopoteza ugenini walipata ushindi wa kwanza katika uwanja ambao leo ndio wanakwenda wa St James Park.

Na kama hujui tu ni kwamba Arsenal hawajawahi kupoteza michezo 5 mfululizo ya ugenini katika calender ya mwaka mmoja tangu wafanye hivyo mwaka 1925, na kama leo watakubali kufungwa itakuwa mara yao ya kwanza ndani ya miaka 93.

Lakini Newcastle wenyewe wanaonekana nj wanyonge sana kwa Arsenal, katika michezo 10 iliyopita ya Newcastle mbele ya Arsenal wamekubali kupoteza michezo yotee mbele ya washika mtutu hao wa London.

Bao la Nolberto Solano mwaka 2005 ambalo liipa ushindi Newcastle mbele ya Arsenal, ndio ushindi wa mwisho kwa Newcastle mbele ya Arsenal na tangu hapo wamekuwa wakichezea kichapo tuu.

Lakini Arsenal huwa wanawafunga Newcastle bao moja tu, na Arsenal wameifunga Newcstle 1-0 kuliko timu yoyote EPL. Michezo 9/26 waliyowafunga Newcastle wamewafunga kwa bao moja tu ikiwemo michezo yao mitati ya mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here