Home Kimataifa Madrid haikubebwa acheni Nongwa

Madrid haikubebwa acheni Nongwa

12916
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Huyu Muingereza Michael Oliver alitoa Penati sahihi kabisa kwa Madrid baada ya Medhi Benatia kumchezea ndivyo sivyo Lucas Vazquez kisha Cristiano Ronaldo kupeleka kilio. Michael Oliver atachukiwa mno na mashabiki wa Juventus kama mmoja wa watu waluomsukuma mgonjwa kabla hajapoteza uhai.

Nimesikiliza makelele na vilio vya walio wengi na ukijaribu kuwasikiliza kwa makini utagundua wengi wao wana chuki. Watu wanalalamikia kumtolewa kwa Gianluigi Buffon. Ni kweli Buffon alistahiki Kadi nyekundu. Alimpotezea muda mwamuzi kwa kumzonga na kumsukuma. Bila shaka alikuwa akitoa kauli chafu. Buffon hakuwa tayari kabisa kumsikiliza Oliver. Je wewe ungekuwa unamwelekeza mchezaji na akiwa anajua kabisa maamuzi hayabadiliki ungefanye? NI HERI MAAMUZI YA KUKAMULIAA JIPU KULIKO KULIACHA LIZIDI KUMEA

Malalamiko ya watu hayaondoi uhalisia wa rafu ya Benatia. Zungukeni popote duniani nitafutieni mahali kuna sheria inayozungumzia HURUMA? Hatukuwa kwenye sanduku la wakatoliki la Maungamo. Ile ilikuwa vita ya Moto na Maji kimojawapo ilibidi kishinde ili moshi uendelee kutawala.

Watu wanalalamikia muda penati iliyotolewa najiuliza kwani Oliver alikuwa anaongozwa kwa ratiba kama mwalimu wa zamu? Aliyekwambia kuna muda wa kutolewa penati ni nani? Ule ulikuwa uamuzi wa busara kabisa wa kumuua muasi aliyetoroka kambini licha ya kwamba alikuwa anakaribia kwenye mpaka wa maadui waliomtuma.

Hivi nyie wajuvi wa mambo tuambieni basi Je Medhi Benatia aliucheza mpira kwa kiungo kipi hicho cha mwili wake? Au wenzetu mna macho ya rohoni? Alimshika mgongoni, bado alirusha mguu kifuani mwake? Je hilo halitoshi kutoa tuta? Najua wengi wenu mna nongwa. Nafahamu chuki na husuda zenu zilikuwa wapi. Sitaki kwenda huko lakini msitake kutuaminisha kuwa mpapai una undugu na mgomba eti kisa mashina yao ni laini Mnataka kuniambia Lucas Vazquez alisukumwa na upepo au siku hizi kuna majini uwanjani?

Nasema kile kinachoshuhudia kutoka moyoni ile ilikuwa ni penati. Roho za wengi zinauma wakitaka Buffon apewe angalau karatasi ya kuibia kwenye chumba cha mtihani ili asipate sifuri. Nikiwa na akili zangu timamu bila unafiki wala unazi Juventus walitisha sana.

Wale wahenga walikuja na moto wa ajabu Bernabeu. Naam. Walitupa burudani haswa. Shida umeme ulikatika na hatupaswi kumlaumu Dijei. Lakini nataka niwaambie akina anko Mbekenyeza kuwa sio kazi ya mwamuzi kukamilisha furaha ya timu fulani. Kazi yake ni kuzitafsiri sheria 17 za fifa kwa uhalali wake pasipo uginingi. Ni kweli aliondoa furaha ile kama upepo wa filimbi yake.

Naelewa hali ya Buffon. Nafahamu fika alivyojisikia. Najua. Nafahamu. INAUMA.

Sawa, lakini Oliver hakuwa na muda wa kurekebisha sheria za fifa pale uwanjani. Labda angeomba udhuru mechi ihairishwe kwa muda. Naami. Hapo tungelewana. Lakini mkisema angeona huruma maana yake mlitaka Oliver abadilishe sheria za fifa kwa wakati ule ule. Ni kweli ana jukumu hilo. Lakini alipaswa kuwashirikisha wenzake kuwa nimepata wazo hapa hapa uwanjani natamani tuone kwa namna gani tunaweza kumsaidia Buffon. Hapo ndipo Buffon angepata bahati na si vinginevyo.

Wengine wanasema mara ooh yule jamaa ni legend mkubwa, alihitaji kuweka historia, unajua ileeee ilikuwaaa mechi yake ya mwisho hivyooo haikuwa vyema kuondoka kwa fedheha hiyo. Shubmaaiiit nani amesema hilo ni jukumu la mwamuzi? Wapi imeandikwa? Wandugu hata mimi naelewa ukubwa na heshima ya Buffon. Fahamu hilo tu. Bila mboyoyo za hapa na pale, eleweni kuwa natambia fila heshima kubwa aliyonayo Buffon na anastahiki pongezi haswa. Yaani sana. Niseme tu ni LEGEND. lakini hakuna sheria inayosema mechi ya mwisho bhana angalieni namna ya kumsaidia Buffon abebe UCL. haipo hivyo. Si sawa.

“SHERIA HAZIBAGUI”

Buffon ni Muitaliano, Oliver ni Muingereza, ulitegemea Oliver angehisi Buffon anaongea nini? Tena si alikuwa amewaka kabisa? Kimsingi tukubaliane tu hata kama aliongea maneno 2000 basi maneno matano ndiyo ya Kiingereza. Sasa alipokosea Buffon, daaah yaani kibaya zaidi alimshikilia na akamnyima mwamuzi uhuru wa kuendelea na mechi. Ndugu zangu UKIWARINGIA MALAIKA KUZIMU INAKUHUSU

Kila mtu aliona wazi kuwa Juve walikuwa wanakimbilia kanisani (Muda wa Nyongeza) hali ilikuwa ngumu kwao na walihitaji daladala kuwahi kufika, bahati mbaya mmoja wao akaomba lifti defenda na mbaya zaid alikuwa na bangi mfukoni (Mehdi) je ulitegemea safari ya kanisani ikamilike kweli?

Nadhani hasira za Buffon zingeenda kwa mabeki walioshindwa kumdhibiti Vazquez Na kumruhusu kutuliza mpira akiwa huru kabisa kwenye boksi. Sitaki kuhusisha tukio hili na fununu za kukosekana kwa waamuzi wa kiingereza kombe la dunia. Hizo mboyoyo zipo sana tu ni kwa vile waingereza wanaonekana sana. Oliver sio mbovu kuzidi hao walioitwa Russia.

Juzi Leroy Sane kakatiliwa goli ambalo lingeipa Manchester City uongozi sa mabao 2-0 dhidi ya Liverpool na hii huenda ingebadilisha kabisa taswira nzima.ya mechi lakini huwezi kusikia mwamuzi Antonio Mateu Lahoz, kutoka hispania akitukanwa tena akiwa ni mmoja wa waamuzi watakao kuwepo Russia.

Niseme tu ukweli wamuuzi wa kiingereza sio wabaya kuzidi wengine ila wao maamuzi yao yanaonekana kwa wepesi zaidi kuliko wengine. Mkitaka kuyaamini haya basi karibuni Russia sio hata mbali kesho kutwa tu hapo. Najua watasaidiwa sana na VAR lakini tutaona mengi. Na nina amini Mark Clutternburg angekuwepo basi angeitwa na hizi lugha zisingekuwepo?

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho kwa mawazo yangu na kwa kuzingatia pia mitizamo na chambuzi mbalimbali za wataalamu wa soka na kuwekea manani maoni ya waamuzi wengine. mwanzoni pia nilijitoa akili kuwa haikuwa sahihi. Sio lazima uamini ninachokiamini lakini huoo ndio mtazamo wangu halali kabisa wa wa mwisho. Pia usisahau kunifollow Instagram (privaldinho) contacts 0763370020

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here