Home UEFA Champions League Warumi ndio kafara ya Liverpool kwenye tambiko la ubingwa

Warumi ndio kafara ya Liverpool kwenye tambiko la ubingwa

11845
3
SHARE

 

AS Roma Vs Liverpool

Kuna uwezekano mkubwa mchezo huu ukawa wa kuvutia zaidi kati ya michezo yote tuliyokwisha itazama hapo awali. Ni mchezo mzuri hasa ukajaribua kuangalia kwa namna AS Roma imepata matokeo muhimu katika michezo yake migumu.

Asante Mungu sio Bayern, Asante Mungu sio Madrid, Alhamdulillah ni Roma. siwadharau Roma, na yeyote anayedhani kuwa hiyo itakuwa mechi rahisi namhurimia sana. hata hivyo hata tungepangwa na nani bado ningesema nafasi ya kusonga mbele ipo kwani huu ni mpira lolote lawezekana”

Hayo sio maneno yangu ni Maneno ya Juggen Klopp

Nikufahamishe tu

Msimu huu AS Roma hajafungwa mchezo wowote katika kiwanja chake cha nyumbani kwenye michuano ya UEFA. wamekuwa na ufanisi mzuri ambao unaleta chachu kubwa katika mchezo huu.

“Nadhani huu ni wakati muafaka wa sisi kufikia lile lengo tulilolitazamia kuwa gumu kwa miaka kadhaa, kiukweli ugumu upo hasa ukiitazamia Liverpool hii ni timu ngumu sana na yenye uwezo mkubwa achilia mbali historia yao katika michuano hii, tunapaswa kujitoa kimasomaso na kuonesha kile tulichokifanya dhidi ya Barcelona haikuwa zali” 

Hayo ni maneno ya mkurugenzi mkuu wa As Roma Bw. Monchi baada ya droo za UEFA.

Ni wazi hawa As Roma wana malengo makubwa sana michuano hii hasa ukiangalia kwa namna walivyobadilika msimu huu kwani wamekuwa na wachezaji wengi wakubwa na Wazoefu (Dzeko, Kolarov, Strootman, Naiggolan n.k).

AS roma wanastahili sio pongezi pia lakini hata kombe hili hasa kwa matokeo ya hapo awali na kwa namna wanavyojitutumua kuhakikisha angalau wanapata kitu. hatupaswi kabisa kudharau kasi na hatupasiw pia kubeza timu yao. Msimu huu imetoa visago mbalimbali katika kiwanja chake cha Nyumbani
As Roma 3-0 Barcelona
As Roma 3-0 Chelsea
As Roma 3-1 Udinese
As Roma 5-1 Benevento
As Roma 3-0 Torino
As Roma 3-1 SPAL
As Roma 3-0 Verona

 

Kwa takwimu hizo ni wazi kuwa wapo vizuri sana katika kiwanja chao cha nyumbani hasa pale inapotokea wakipata nafasi wanazitumia vyema. Kwenye kiwanja chao cha nyumbani imeshinda michezo 9 imesuluhu 1 na kufungwa michezo 6. Kwenye msimamo wa ligi wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 60. Kwenye safu ya kiungo wana mchezaji murua kabisa Radja Naiggolan ambaye atakutana na mchezaji mwenzake kutoka taifa ya Ubelgiji Simon Mignolet. Kiungo mwingine hatari ni Kevin Strootman

Ubora wa Mo Salah na Dzeko
Mo Salah Edin Dzeko
Magoli 29 22
Wastani wa Mashuti 3.74 4.23
asisti 11 6
ujuzi 7/10 4/10
Nafasi 55 43
Pasi 76% 71%

 

Ubora wa Liverpool upo zaidi kwenye safu yake ya ushambuliaji.
Jina Ligi kuu FA UEFA jumla
Mo salah 29 1 9 39
Firmino 14 1 9 24
Mane 9 0 7 16

 

Safu hii ya ushambuliaji imekwishafunga magoli 79 msimu huu idadi kubwa kuliko magoli yaliyofungwa na klabu yoyote kwenye ligi kuu Italia kwenye mashindano Serie A. pia idadi hii ni kubwa kwa As roma katika michuano yote. Hii inaweza kuwa hatari kubwa zaidi kwa Roma kwani wamekuwa na rekodi mbaya katika uzuiaji kwani kwenye mechi za ligi nyumbani imeruhusu kufungwa michezo 6.

As Roma wamekuwa na matokeo mabovu sana nyumbani licha ya kwamba wamefanya vizuri pia?
Roma 1-3 Inter
Roma 0-0 Napoli
Roma 1-2 Atlanta
Roma 0-1 Sampdoria
Roma 0-2 Ac Milan
Roma 0-2 Fiorentina
Pia kutakuwepo na Shida  kwa upande wa Liverpool kuhakikisha kuwa watamzuia Edin Dzeko kufunga hasa baada ya kuonesha kiwango maridhawa katika michezo yake kadhaa ya UEFA dhidi ya Chelsea na Barcelona.

“Ni matumanini yangu kuwa tutasonga mbele, hakuna hata mmoja aliyeamini kuwa tutafika hapa, kwa mara yangu ya kwanza katika hatua ya nusu fanili ya UEFA, nina furaha sana leo naitazama Roma kwenye droo ya hatua ya nusu fainali” Edin Dzeko

Liverpool nayo imekuwa na safu ya ulinzi mbovu kabisa kwani imeruhusu magoli 33 kwenye msururu wa michezo ya ligi kuu England.

Bila shaka hutapingana nami kuwa huu ndio mchezo wa kuvutia zaidi hasa ukijaribu kuangalai naman takwimu za pande zote mbili zinavyolandana.

Roma nao watakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha Mo salah aliyeiangamiza Man City kutokufanya maajabu mengine. katika kipinid cha Hivi karibu Mo salah ametwa tuzo ya mchezoaji bora wa mwezi mara 4, huku katika wiki ya kwanza ya hatua yha robo fainali alipewa tuzo ya mchezaji bora wa wiki wa UEFA. Wiki ya Mwisho pia Sadio Mane nae ametwaa mchezaji bora wa wiki wa UEFA. Mtiririko huu wa Liverpool ni si haba na watahakikisha wanapasi nguo mapema kabla umeme haujakatika.

PATA KIFURUSHI Matokeo walipokutana mara ya mwisho
TAREHE MECHI UBAO MASHINDANO
30 May 1984 AS Roma v Liverpool 1-1 European Cup
15 Feb 2001 AS Roma v Liverpool 0-2 UEFA Cup
22 Feb 2001 Liverpool v AS Roma 0-1 UEFA Cup
05 Dec 2001 AS Roma v Liverpool 0-0 UCL
19 Mar 2002 Liverpool v AS Roma 2-0 UCL
Roma walipata nafasi ya kipekee kuifunga Barcelona ambayo ilionekana kuitawala sana mchezo wa marudiano katika uwanja wa Stadio Olympico. wengi walitazamia Barcelona kutinga hatua hii lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo

Hakuna haja ya kuongojea miujiza tena ni muda wa kuhakikisha tunasonga mbele haraka iwezekanavyo” Daniel De Rose

 

Liverpool vs Roma
Liverpool v Roma: Jumatano, 24 April (04:45)
Roma v Liverpool: Jumatano, 2 May (04:45)

MTAZAMO WANGU?

Kwanza nina imani kubwa kuwa Liverpool inaweza kutwaa ubingwa huu. Liverpool ni timu mzuri sana. Ujio wa Van Djik ni tiba mbadala. Hapo mwanzo chakula cha Liverpool kilikosa Chumvi. Djik ameleta ile ladha ambao walio wengi waliitarajia. Ukiachilia mbali uzuri wake, bado Djik ana deni, deni hilo ni kuzuia tembo (Dzeko). Ni kweli amefanikiwa kuzuia nyani (Gabriel Jesus) lakini je ataweza kuzia na tembo? Faida ya Liverpool ni kocha waliye nae. Klopp tayari amekwisha fika hatua ya Fainali akiwa na klabu iliyokuwa haitazmiwi pia kufika hatua hiyo. hivyo nina imani kubwa kuwa anaweza kufanya hivyo pia. wengi hawakuipa nafasi sana Liverpool lakini nilitabiri tokea awali Liverpool anaweza kutwaa ubingwa huu. Kwa Takwimu hizi napeleka karata yangu kwa Liverpool kusonga mbele, je wewe una mtazamo gani.
Makala hii imeandaliwa na Privaldinho (unaweza pia kunifollow Instagram)

Comments

comments

3 COMMENTS

  1. Makala nzuri ila hii mechi ya Liverpool na roma ni mechi ngumu sana pengine kuliko bayen na Madrid Cz hawa wote wanataka kuitambulisha dunia kuwa wanaweza kufanya kitu hasa kutokana na watu wengi kutozipa nafasi timu hizi kufika hapa zilipofika
    Sor kwa mtazamo wangu ni mechi ngumu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here