Home Kitaifa Sababu ya Waziri Ummy kuingia Coastal Union imetajwa

Sababu ya Waziri Ummy kuingia Coastal Union imetajwa

7300
1
SHARE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amefafanua sababu zilizopelekea kuingia kwenye soka na kuisaidia Coastal Union kurudi tena ligi kuu Tanzania bara.

Mh. Mwalimu amesema kwa sasa wanatafuta wachezaji wenye uwezo wa kucheza ligi kuu pamoja na kutafuta mbinu mbalimbali za kuiongeza klabu yao mapato ikiwa ni pamoja na kutafuta wadhamini.

“Jambo kubwa ambalo tunalifanya kwa sasa pamoja na uongozi wa timu ni kusajili wachezaji ambao wataweza kucheza ligi kuu tanzania bara, uongozi pia unapanga namna ya kuinua mapato kwa kutafuta wadhamini na wadau ambao wataisaidia timu ili ifanye vizuri ikiwa ligi kuu.”

“Tumeangalia pia ili Coastal iweze kurudisha heshima yake kama zamani  ni kuhakikisha inakuwa na uwanja wake wa kufanyia mazoezi na hostel za wachezaji na nimepata mdau ambaye alinichangia kwa nipa eneo ambalo tumewapa Coastal ambapo tunategemea kujenga kiwanja na hostel za wachezaji.”

“Tunaendelea kuwandaa kisaikolojia wakazi wa jiji la Tanga na timu nyingine ambazo zinashiriki ligi kuu kwamba Coastal Union inakuja kwa ajili ya kutoa ushindani katika ligi kuu na hatutaki kuwa washiriki tu, ikiwezekana tutatwaa kombe kama ilivyokuwa mwaka 1988.”

Amesema sababu kubwa ya Coastal Union kushindwa kufanya vizuri kwenye ligi na kushuka daraja mara kwa mara imekuwa ni ugomvi na makundi ndani ya timu hiyo.

“Sababu kubwa ni ugomvi wa ndani unaosababishwa na makundi lakini nashukuru kila kiongozi wa klabu na viongozi wengine wa Tanga tumeliona na kukubaliana tuwe wamoja baada ya timu kurudi ligi kuu na umoja na mshikamano wa wanatanga ndio umepelekea timu imepanda.”

Comments

comments

1 COMMENT

  1. TUMERUDI TENA WAGOSI WA KAYA{COASTAL UNION} WADAU WA SOKA MKOANI TANGA TUIPE SAPOTI TIMU YETU YA TANGA PEKEE ILIYOBAKI LIGI KUU TANZANIA BARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here