Home Kitaifa Je wajua? Okwi, Bocco wamefunga magoli mengi zaidi ya timu 14 VPL

Je wajua? Okwi, Bocco wamefunga magoli mengi zaidi ya timu 14 VPL

10393
0
SHARE

Alhamisi Aprili 12, 2018 Emanuel Okwi na John Bocco walifunga goli moja kila mmoja kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City mchezo ambao Simba ilishinda 3-1 uwanja wa taifa.

Okwi alifikisha magoli 18 na Bocco aliunga goli lake la 13 na kufanya wawili hao kuwa na magoli 31 kwa pamoja. Pacha ya Okwi na Bocco ndiyo imefunga magoli mengi zaidi kwenye ligi hadi sasa pamoja na timu yao.

Magoli yao 31 yanawafanya kuwa na idadi kubwa ya magoli kuliko timu 14 za ligi kuu, ukiachana na Simba, Yanga ndiyo timu pekee inayowazidi kwa magoli (Yanga imefunga magoli 39 baada ya kucheza mechi 22)

Timu ambazo zimezidiwa magoli na Okwi na Bocco kwa pamoja ni Mwadui (26) Azam (24), Tanzania Prisons (22), Singida United (22), Mbeya City (21), Mbao (21), Majimaji (21), Ruvu Shootung (20).

Nyingine ni Mtibwa Sugar (19), Lipuli (17), Stand United (16) Ndanda (16), Kagera Sugar (15) na Njombe Mji (14).

Okwi peke yake amefunga magoli mengi zaidi ya magoli yote yaliyofungwa na Lipuli (17), Stand United (16) Ndanda (16), Kagera Sugar (15) na Njombe Mji (14).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here