Home Kitaifa Eeh! Kumbe Waziri Ummy ‘Mnyama’ damu

Eeh! Kumbe Waziri Ummy ‘Mnyama’ damu

9951
0
SHARE

Kama ulikuwa hujui basi nakujuza kuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ni shabiki wa kindakindaki wa Simba ‘Mnyama’ tangu kitambo hicho halafu akiwa Tanga ni shabiki wa African Sports.

Ummy Mwalimu amesema amesema ameingia Coastal Union kwa sababu ya nafasi yake ya uongozi, hawezi kubagua timu kwa sababu yeye ni kiongozi wa wanatanga wote bila kujali vitu vinavyowatofautisha.

“Nipo very active Simba tangu zamani na Tanga nilikuwa nashabikia African Sports kwa sababu baba yangu ni shabiki wa timu hiyo lakini sasa Coastal kwa sababu ya nafasi ya uongozi huwezi kubagua kwa kusema mimi ni African Sports.”

“Mimi ni shabiki wa michezo lakini pia baada ya kazi napenda kufurahi, kama unakumbuka nilishabikia Twiga wakati wanacheza mwaka 2012 lakini pia ni shabiki wa Simba.”

“Niliingia Coastal kwa sababu ya kuguswa na taarifa ambazo viongozi walinipa kwa kuniambia Mh. Waziri tusipopanda msimu huu, hatupandi tena tunaomba support yakokwa hiyo kama kiongozi nikaona nina wajibu wa kusukuma ili Coastal ipande.”

“Kilichonivuta zaidi ni kwamba, Coastal kucheza  ligi kuu ni kuinua pia hali ya kiuchumi na kijamii ya wakazi wa jiji la Tanga.”

Coastal United itacheza ligi kuu Tanzania ikiwa ni miongoni mwa timu nne zilizopanda daraja kutoka ligi daraja la kwanza, timu nyingine ni Biashara ya Musoma, Alliance Schools ya Mwanza na JKT Tanzania ya Dar.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here