Home Kitaifa Azam yakwama Mlandizi

Azam yakwama Mlandizi

8365
0
SHARE

Ligi kuu Tanzanua bara imeendelea leo Aprili 13, 2018 kwa mchezo mmoja uliochezwa uwanja wa Mabatini-Mlandizi ambapo Ruvu Shooting ilikuwa ikiialika Azam, dakika 90 za mchezo huo zimemalizika kwa Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Goli la kwanza la Ruvu Shootung limefungwa dakika ya 29 na mchezaji wa zamani wa Azam Hamisi Mcha huku goli la pili likifungwa na Fully Maganga dakika ya 80.

Afisa habari wa Azam Jafar Idd amekubali matokeo hayo na kusema kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Azam Complex.

“Tumefungwa 2-0 na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini, awali mchezo huu ulikuwa uchezwa jana lakini mvua kubwa ikasababisha tushindwe kucheza mchezo umechezwa leo.”

“Wenzetu walipata nafasi mbili wakazitumia sisi tukapambana kadiri ya uwezo wetu lakini hatukuwa  na bahati ya kufunga magoli kwenye mchezo wa leo.”

“Makosa ambayo yamejitokeza kwenye mchezo wa leo mwalimu atayafanyia kazi na tutarejea tena kwenye mchezo wa ligi siku ya Jumapili katika uwanja wa Azam Complex ambapo tutakutana na Njombe Mji.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here