Home Kimataifa Arsenal waangukia kinywani mwa Atletico Madrid, Marseille wapewa Red Bull tena

Arsenal waangukia kinywani mwa Atletico Madrid, Marseille wapewa Red Bull tena

9331
0
SHARE

Ni Atletico Madrid vs Arsenal nusu fainali Europa. Hizi ndio timu mbili ambazo zinapewa nafasi kubwa kutwaa michuano ya Europa mwaka huu, mchezo huu unaonekana kama fainali ambayo inachezwa katika nusu fainali.

Arsenal wana kumbukumbu nzuri katika nusu fainali dhidi ya timu kutoka Hispania, mara ya mwisho kwa Arsenal kukutana na timu kutoka Hispania katika nusu fainali ilikuwa 2005/2006 vs Villareal na Arsenal walishinda.

Lakini kama ilivyo kwa Arsenal, Atletico Madrid nao wana rekodi nzuri nusu fainali dhidi ya timu toka Uingereza, msimu wa 2009/2010 Atletico walifanikiwa kuitoa Liverpool kwa goli la ugenini katika hatua kama hii.

Na kama hujui tu ni kwamba Arsenal ndio timu ya 5 toka EPL kuwahi kucheza nusu fainali ya Champions League, nyingine ni Fulham, Liverpool, Chelsea na Manchester United.

Katika nusu fainali nyingine ya Europa League Marseille atacheza dhidi ya RB Salzburg, Marseille amekwenda nusu fainali baada ya kuitoa timu inayodhaminiwa na Raed Bull(Rb Leizpg) na anakwenda kukutana na timu nyingine ya Red Bull.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here