Home VPL Yanga Vs Singida: Mashabiki wa Yanga mmekwama wapi?

Yanga Vs Singida: Mashabiki wa Yanga mmekwama wapi?

7314
0
SHARE

“Nenda kamuulize akilimali yeye ndiye mwenye majibu sio sisi, tena nyie waandishi wa habari tusiwaone maana mbagua taarifa”

haya yalikuwa maneno ya mshabiki mmoja aliynifuata kwa ghadhabu kubwa maraa baada ya mchezo wao dhidi ya Singida kuisha. Ni wazi kuwa walikuwa na hasiria kubwa sana hasa baada ya matokeo. Wengine walikuwa tayari kutaka kunipiga ila baadhi walitumia busara zao na kupunguza rabsha ile. Nilikuwa nafanya mahojiano na mashabiki lakini ghafla tafrani ilizuka wakitaka niwafate viobfozi wa Yanga kuwahoji. Enewei viongozi wa Yanga mnatafutwa namashabiki wenu. Wamesema nyie ndio mna majibu sahihi kuhusu mwenendo wa Timu yao.

Mchezo kwani ulikuwaje?

Yanga kipindi cha kwanza waliruhusu goli la mapema mno ambalo liliharibu hali ya hewa. Singoda walicheza kwa uangalifu mkubwa na hawakuwa na haraka sana na walikuwa wakipiga pasi nyingi za kuwazubaisha Yanga.

Walinda lango?

Youthe Rostand hakupata kashkashi sana na alitulia vyema golini. Alionekana mara kadhaa kuipandisha timu na kujaribu kuinua morali ya timu. Mlinda mlango wa Singida Mustapha Barthez aliokomoa michomo miwili kabla ya kupata majeraha na kumpisha Manyika Jr ambaye aliondosha shambuli moja la hatari kabla hajaokomoa mchomo wa Ibrahimi Ajibu.

Safu ya Ulinzi

Safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa imetulia vizuri sana leo licha ya makosa ya awali. Mshambuliaji wa Singida kambale amekiri mwenye alipata sana ugumu

“niliteseka sana kwani nilikuwa mwenyewe na nilikabwa na walinzi wawili” alisema

yanga waliondosha mashambulizi ya hatari mara saba, Singida waliondosha mashambulizi kwenye eneo lao mara 15. Yanga walibloku mipira miwili tu ya hatari huku safu ya ulinzi ya Kenedy na Antir ikibloku mipira 13 kwenye eneo lao la hatari.

Umiliki wa mpira na safu ya kiungo

Singida waligusa mpira mara nyingi zaidi hasa katika eneo lao la nusu ya uwanja. Mwalimu wa Singida alifahamu udhaifu wa Yanga ni upi na alitumia mbinu yake ya kuuficha mpira ili kuwavuruga Yanga. Walicheza mipira mirefu ambayo mingi ilikuwa ya kubadili uwanja na sio kutengeneza mashambulizi. Msimamo wao ulikuwa kutokuruhusu mpinzani wake (nsajigwa) kupata mpira.

Ufafanuzi

Mwandishi: kukosekana kwa Mwalimu Lwandamila je kumeathiri mchezo wa leo

Nsajigwa: siku zote baba mwenye nyumba akiondoka uwezekano wa familia kuyumba pia upo.

Safu ya ushambuliaji

Yanga walionekana wazuri hasa kwenye lango la Singida kwani walitengeneza mashambuli ya hatari mara 79 huku Singida wao wakitengeneza mashambulizi 44.

PATA KIFURUSHI

Takwimu kwa ujumla

kona Mashuti waliotea Kadi Njano
Yanga 7 8 (2) 3 1
Singida 4 5 (1) 2 2

Mchezaji wa Singida alipohojiwa kuhusu mchezo huu alisema. Tumetoka sare kwa sababu Yanga na Singida tumejuana sana na tumefahamiana hivyo mbinu zetu zilikingiana kifua.

Nahodha ya Yanga anena

Wachezaji wamepambana wameonesha uchu wa kutaka kushinda lakini mwisho wa mchezo tumetoka sare ila hilo halikuwa lengo letu, maana washambuliaji wetu walipata nafasi lakini hawakuweza kuzitumia. Kusema ukweli inauma kwa sababu sisi tulishazoea kushinda kila mchezo tunamwachia na Mungu ndio ameshasema tuwe droo. Nguvu zetu kwa sasa ni kwa Ethiopia ili kuwakilisha vizuri taifa.

Ila nazidi tu kuwakumbusha mashabiki wa Yanga, waandishi wa habari ndio wanaotumika kufikisha ujumbe wenu kwa wahusika. Mkileta chuki baina yetu haisaidii. Waandishi hawahusiki sana na timu yenu kuyumba au kushindwa kupata matokeo chanya. Mkifungwa sisi tunaingia vipi? Maana malalamiko yenu makubwa ni kw viongozi na ukata. Au sisi ndio tumemuondoa Lwandamina? Msiwe na gubu wala Nongwa. Msihamishie hasira zenu kwetu. Kama kuna gazeti au chombo kinachafua timu yenu nendeni kwenye taaisisi husika ili wengine tuendlee kufanya kazi kwa amani. Ni hayo tu.

Imeandaliwa na Priva Abiud (unaweza pia kunifollow Instagram Privaldinho)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here