Home Kimataifa Wasikilize wachezaji wa Juve na raisi wao wanasemaje kuhusu tukio la jana

Wasikilize wachezaji wa Juve na raisi wao wanasemaje kuhusu tukio la jana

12430
0
SHARE

Huzuni, furaha, hasira ndio zinaufanya mchezo wa soka kuwa mchezo mtamu sana, wakati mashabiki na wachezaji wa Real Madrid wakishangilia kuhusu ushindi wao wa jana hali ni tofauti sana kwa Juventus.

Medhi Benatia ambaye ndio chanzo cha penati hiyo amesema “iko wazi na hata ukiangalia niliugusa mpira kwanza na ukabadili muelekeo, Lucas Vazquez alipoona hana la kufanya akajiangusha, inaumwa kwa kuwa mwaka jana ilitokea hivi hivi kwa Bayern Munich”

Giorgio Chiellini anasema “sio jambo la kushtua kwa kuwa Bayern nao walifanyiwa hivyo hivyo mwaka jana na leo ni zamu yetu(kuhusu maamuzi tata Santiago Bernabeu) Real hawakutarajia tunaweza kubadili matokeo na kwa alichofanya muamuzi unabaki tu unashangaa.
Andrea Agnelli raisi wa Juventus naye anasema “kwanini VAR haitumiki CL, inaonekana kama kuna mpango wa aina ya marefa kama hawa ambao wanapewa kazi kuzimaliza timu za Itali, angalia Ac Milan dhidi ya Arsenal na sisi leo tumekuja kufanyiwa hivyo hivyo”
Gianluigi Buffon “huwezi ukakatisha ndoto za mwanadamu mwenzako kwa namna ile, unakuwa huna huruma na kama mtu hawezi kuja uwanjani katika namna hii no bora ukae jukwaani unywe soda na mkeo muangalie mpira”
Lakini Lucas Vazquez ambaye ndio alichezewa faulu ana lake pia la kusema  “ni suala lisilo na mjadala, wakati naufuata mpira nilisikia mlinzi wao anakuja nyuma yangu na kunisukuma, ni kawaida wao kuumia kwa kuwa tukio lilitokea katika dakika za mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here