Home Kitaifa Simba inajitofautisha na Yanga

Simba inajitofautisha na Yanga

10180
0
SHARE

Simba inaendelea kujitofautisha na Yanga kwenyebmsimamo wa ligi kuoka na pointi za vilabu hivyo. Mnyama amefikisha pointi 55 baafa ya kupata pointi tatu kutoka kwa Mbeya City kufuatia ushindi wa magoli 3-1 na kuiacha Yanga kwa pointi nane.

Simba ikiwa imecheza mechi 23, Yanga ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 lakini imecheza mechi 22.

Magoli ya Simba yamefungwa na Emanuel Okwi, Asante Kwasi na John Bocco, goli pekee la Mbeya City limefungwa na Fank Ikobela.

Vita ya ubingwa wa VPL imefika patamu, Simba na Yanga kwa pamoja kila timu bado ina nafasi. Yanga imebakiza mechi nane Simba imebakiza mechi saba.

Endapo Simba itaendelea kushinda hadi meisho bila shaka itanyanyua taji la ligi lakini Yanga bado ipo kwenye mbio za ubingwa kwa sababu ikiendelea kushinda mechi zilizobaki ikiwemo mechi ya watani wa jadi itajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea taji lao.

Nahodha msaidizi wa Simba Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mchezo wa leo ulikuwa muhimu kupata magokeo kuelekea ubingwa.

“Mechi yaleo ilikuwa ni muhimu sana kwetu kupata matokeo kuelekea kwenye ubingwa.”

Golikipa wa Mbeya City Owen Chaima anaamini watasalia kwenye ligi kwa ajili ya msimu ujao licha ya kwamba timu yao ipo kwenye nafasi ya hatari.

“Nafasi bado ipo hatuwezi kukata tamaa hadi mwisho tumebakiza michezo mingine ambayo tutaitumia kuakikisha tunabaki kwenye ligi.”

“Mipindi cha kwanza tuliruhusu magoli matatu lakini kipindi cha pili tulikuwa vizuri kuliko kipindi cha kwanza ndio maana hatukuruhusu goli.”

Mbeya City ipo nafasi ya tisa (9) kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 26 sawa na Mwadui na Ruvu Shooting. Stand United ina pointi 25, ikifuatiwa na Ndanda, Kagera Sugar na Mbao ambazo kwa pamoja zina pointi 23.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here