Home Kimataifa Sababu 4 ambazo Shaffih Dauda anaamini zimeigharimu Barcelona

Sababu 4 ambazo Shaffih Dauda anaamini zimeigharimu Barcelona

11129
0
SHARE

Michezo ya robo fainali ya Champions League imekwisha, Real Madrid, Liverpool, As Rom na Bayern Munich wanakwenda nusu, lakini kuondolewa kwa Barcelona kumekuwa habari kubwa zaidi wiki hii.

Mchambuzi nguli wa masuala ya michezo Tanzania Shaffih Dauda naye ana mtazamo wake, akiongea kupitia kipindi cha Sports Extra Shaffih alisikika akisema sababu zifuatazo kuwa ndio ziliigharimu Barcelona na kuifanya Roma kwenda nusu fainali CL kwa mara ya kwanza tangu 1983/1984.

1.Pengo la Neymar. Barcelona bado wanaonekana kuhangaika kuziba pengo la Mbrazil huyu, wakati Barcelona wakiwa na Neymar kazi ilikuwa rahisi sana katika eneo lao la ushambuliaji.

Wakati Barcelona wakipindua kipigo cha 4-0 pale Nou Camp kwa mfano Neymar alikuwa Man Of The Match, lakini katika mchezo dhidi ya As Roma Barcelona walionekana wazi kuimiss huduma ya Neymar na kumfanya Messi kuonekna mtumwa uwanjani.

2.Man to Man style ya As Roma. Kelvin Strootman, Kostas Manolas, Radja Nainggolan na wachezaji wote wa As Roma walionekana kucheza na mtu mmoja mmoja wa Barcelona, hii iliwafanya muda mwingi kukosa uhuru wa kuchezea mpira na ikawafanya As Roma kuwa huru kufanya watakacho.

3.Philippe Coutinho na wachezaji wapya. Wakati huu ambapo Neymar hayupo ndipo wachezaji wapya walipaswa kuonesha umuhimu wao, Philippe Coutinho hana kibali bado kuichezea Barcelona katika CL na wachezaji wengine wapya bado hawaoneshi uwezo mkubwa.

Wakati Coutinho yeye akiwa bado hajaanza kuitumikia Barcelona, maingizo mapya kama Nelson Semedo pamoja na Yerry Mina wenyewe ndio kwanza wanaonekana kutowapa Barcelona kile walichokitaraji toka kwao.

4.Samuel Umtiti. Eneo la ulinzi la Barcelona limekuwa likicheza vibaya siku za usoni, Samuel Umtiti amekuwa hana kiwango kizuri msimu huu, Sergio Busquet ameanza kupwaya ukabaji wake na walinzi wengine wa Barcelona wameonesha wazi ubovu wao dhid ya As Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here