Home Kimataifa Ona magazeti ya Italia yalivyotokwa povu hii leo asubuhi, hukunya Hispania yakijibu

Ona magazeti ya Italia yalivyotokwa povu hii leo asubuhi, hukunya Hispania yakijibu

11006
0
SHARE

Ni kati ya wiki bora sana za Champions League, siku zote mbili kumekuwa na matukio makubwa. Tukio la penati waliyopewa Real Madrid limekuwa gumzo kubwa ulimwenguni hii leo kiasi cha magazeti ya Italia na Hispania kuibuka na vichwa vya habari tofauti.

Corriere Dello Sport la nchini Italia leo limeamka na kichwa cha habari kinachosomeka “Che Furto” ikimaanisha “Robbery” yani kwa lugha ya kwetu ni kitendo cha kama ukabaji au wizi, wakimaanisha Juve wamefanyiwa Robbery na muamuzi.
Hawakuishia hapo bali chini ya kichwa cha habari wakaandika “penati dakika ya 93, Buffon ametolewa nje, muamuzi anapaswa kuona aibu” moja kwa moja habari hii inaonesha kumshambulia muamuzi Michael Oliver wa Uingereza.

Gazeti la Sport la nchini Italia nalo limeandika “El Robo Del Siglo” hii ikiamaanisha “The theft of the Century” kwa lugha ya kwetu wanasema “Ulikuwa ni wizi wa karne” waliofanyiwa Juventus na Michael Oliver.

Gazeti la As nalo leo asubuhi kichwa chake cha habari kiliandikwa “Del Panico A La Semifinal” na hii ilimaanisha “Panic to the Semi Final” likimaanisha mvutano kati ya Juve na Real Madrid kuelekewa nusu fainali.

Sasa hao ni Italia, kule nchini Hispania gazeti maarufu la michezo la Marca limeungana na muamuzi Michael Oliver na wameandika kichwa cha habari kinachosomeka kwa kingereza “It was a Penalty” huku wakiweka picha ya Mehdi Benatia akioneka kwa nyuma kumgusa Lucas Vasquez.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here