Home Kimataifa Mkufunzi wa waamuzi CAF atoa ufafanuzi kuhusu penati ya Real Madrid na...

Mkufunzi wa waamuzi CAF atoa ufafanuzi kuhusu penati ya Real Madrid na kadi ya Buffon

19500
0
SHARE

Mjadala wa tukio la jana wakati wa mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus bado unaendelea, penati ya dakika za lala salama waliyopewa Real Madrid na kadi nyekundu ya Gianluigi Buffon ni mjadala mzito sana.

Tuanze na penati, mkufunzi wa waamuzi wa shirikisho la soka barani Africa Leslie Liunda ametoa mtazamo wake kuhusu penati ya Real Madrid na kwa upande wangu maelezo ya Liunda yemetoa jibu la wazi kabisa kuhusu penati ile.

Liunda kwanza anatoa tafsiri ya namna mpira Benatia alivyoucheza, Benatia alikuwa nyuma ya Vazquez, ina maana Vazquez alikuwa katikati ya mpira na Benatia, ina maana kama ukiwa nyima ukitaka kuucheza mpira mbele ulio mbele ya mtu lazima uurukie na umrukie mchezaji, na kitendo cha kumrukia mchezaji ni penati.

Pili, mpira ulikuwa ni wa kucheza kwa kifua kama ilivyoonekana wakati Vazquez anaufuata lakini Benatia aliucheza kwa miguu. Tukio la kucheza mpira wa kichwa au kifua kwa miguu moja kwa moja ni faulu na Michael Oliver alifanya hivyo.

Lakini pia kwa namna ambavyo Benatia aliufuata mpira alionekana kumbughudhi Vazquez, alionekana kumnyima uhuru wazi wazi wa kuumiliki mpira na kuweka mkono mgongoni mwa Vazquez lilikiwa tuta la waziwazi.

Kuhusu kadi nyekundu, Leslie Liunda anasema tukio walilofanya Buffon na wachezaji wenzake wa Juventus baada ya uamuzi wa penati lilikuwa la kawaida kutokana na presha ya mchezo na dakika penati ilipotolewa. Refa alikosa busara kwa kushindwa kujiandaa kukabiliana na mhemko huo akatoa kadi nyekundu.

Shaffih Dauda kwa upande wake hakubaliani na wanaosema Buffon hakustahili kadi nyekundu. Dauda anaamini kwa reaction ya Buffon baada ya filimbi ya penati ni wazi alimuambia muamuzi maneno mabaya na alipaswa kutolewa nje bila kujali kwamba yeye ni nahodha au laa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here