Home Kitaifa Yanga vs Singida ni kufa au kupona

Yanga vs Singida ni kufa au kupona

7765
0
SHARE

Leo Yanga itacheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Singida United kwenye uwanja wa taifa Dar. Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote ile kuweka hai matumaini yake ya kutetea taji la VPL.

Yanga ipo nyuma ya Simba kwa pointi sita, Wekundu wa Msimbazi wamefikisha pointi 52 baada ya ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar huku Yanga ikiwa na poini 46 kabla ya mchezo wa leo ambao utakuwa ni wa 22.

Ushindi utaifanya Yanga kupunguza gape la pointi kutoka sita hadi tatu huku timu hizo mbili (Simba na Yanga) zikiwa sawa kwa mechi za kucheza (22). Endapo Yanga itapoteza mchezo wa leo itaendelea kubaki nyuma ya Simba kwa pointi sita, lakini ikitoka sare itabaki nyuma kwa pointi tano.

Yanga imeshindwa kupata matokeo mbele ya Singida United katika mechi za hivi karibuni, tangu Singida imerejea ligi kuu kwa mara nyingine timu hizo zimekutana mara nne. Yanga imeshinda mechi moja, sare mbili na Singida imeshinda mechi moja.

Mchezo wa leo ni mgumu kwa kila upande, Singida haijapata matokeo uwanja wa taifa katka mechi mbili zilizopita. Ilifungwa na 3-2 na Yanga kwenye mechi ya kirafiki kabla ya Simba kuifunga 4-0 kwenye mchezo wa ligi.

Yanga inahitaji kulipa kisasi kwa Singida kufuatia kufungwa kwa penati 4-2 kwenye mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup na kutupwa nje ya mashindano hayo. Singida wanahitaji kuendeleza ubabe wao kwa Yanga na kujenga heshima kwenye soka nchini.

Taarifa mbaya kwa Yanga ni kuondokewa na kocha wao mkuu George Lwandamina, koha huyo ameondoka kwa kushtukiza wakati Yanga inapigana kutetea taji la ligi.

Kuondoka kwa kocha huyo kunaweza kuiathiri Yanga kiufundi na kisaikolojia. Lwandamina alikuwa kocha mkuu, mbinu na ufundi wake ndani ya kikosi ndio kuimeifikisha hapo ilipo lakini inawezekana wachezaji wakakosa kujiamini wanapokutana na timu yenye kocha anaeifahamu vyema timu yao huku wao wakicheza bila kiongozi wa benchi la ufundi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here