Home Kitaifa Yanga maumivu juu ya maumivu

Yanga maumivu juu ya maumivu

8702
0
SHARE

Yanga wakati bado wanauguza maumivu ya kuondokewa na kocha wao mkuu George Lwandamina wameingia kwenye maumivu mengine ya kupoteza pointi mbili kufuatia sare ya kufungana 1-1 na Singida United katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Lwandamina hakuwepo kwenye benchi la ufundi la Yanga wakati ikicheza mechi ya leo dhidi ya Singida United na kocha huyo ameshatangazwa kuijiunga na timu yake ya zamani ZESCO United ya Zambia.

Sare ya leo inaweka Yanga nyuma ya Simba kwa pointi tano baada ya timu zote kucheza mechi 22 na kubakiza mechi nane kabla ya ligi kufikia ukingoni. Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 52 huku yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointi zake 47.

Magoli katika mchezo wa leo yamefungwa na Kambale Salita aliyeifungia Singida dakika ya pili kipindi cha kwanza, Shaibu Abdallah ‘Ninja’ akaisawazishia Yanga 45+2.

Yanga haijapata matokeo dhidi ya Singida United kwenye mchezo wowote wa mashindano rasmi, timu hizo zimekutana mara nne kwenye mashindano rasmi, Singida imeshinda mara moja, michezo mitatu imemalizika kwa sare.

  • 04/11/2017 Singida United 0-0 Yanga (VPL)
  • 08/01/2018 Singida United 1-1 Yanga (Mapinduzi Cup)
  • 01/04/2018 Singida United 1-1 pt 4-2 (ASFC)
  • 11/04/2018 Yanga 1-1 Singida United (VPL)

Mchezo pekee ambao Yanga ilishinda dhidi ya Singida United ulikuwa wa kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi. Yanga ilishinda  3-2 uwanja wa taifa Agosti 5, 2017.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo Aprili 11, 2018

  • Stand United 1-3 Majimaji
  • Mbao 2-1 Njombe Mji
  • Tanzania Prisons 1-1 Kagera Sugar
  • Mwadui 2-1 Lipuli

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here