Home Dauda TV Video-Makomando Singida, Yanga walivyoshikana mashati kabla ya mechi

Video-Makomando Singida, Yanga walivyoshikana mashati kabla ya mechi

5349
0
SHARE

Imekuwa ni jambo la kawaida sasa kwa baadhi ya vilabu vya ligi kuu kutumia makomandoo kwenye viwanja mbalimbali zinapochezwa mechi za mashindano mbalimbali. Makomando hao inaelezwa kazi yao ni kulinda usalama wa wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Kabla ya mchezo wa Yanga vs Singida United kuanza, uliibuka ‘mtiti’ kati ya makomandoo wa timu hizo, chanzo cha ugomvi huo ilikuwa makomandoo wa Yanga walikuwa wakiwazuia makomandoo wa Singida United kuingia uwanjani jambo ambalo lilizua kizaazaa kwenye geti la kuingilia uwanjani kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Polisi ilibidi waingilie kati vurugu hizo ambazo zilianza kupamba moto huku baadhi yao wakimwagiana maji na kukunjana mashati, hakuna aliyejeruhiwa kutokana na vurugu hizo ambazo baadaye zilidhibitiwa na jeshi la polisi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here