Home Dauda TV Video-Cannavaro amezungumzia nafasi ya Yanga kutwaa ubingwa VPL na mechi ya Simba...

Video-Cannavaro amezungumzia nafasi ya Yanga kutwaa ubingwa VPL na mechi ya Simba na Yanga

7756
0
SHARE

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema anaamini timu yake bado ina nafasi ya kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu mbele ya Simba ambayo hadi sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Yanga baada ya ‘wana Jangwani’ kutoka sare ya kufungana 1-1 na Singida United.

Cannavaro amesema pointi tano ni nyingi lakini ili kumfukuza mpinzani wako lazima uwe unashinda mechi zako, pia akaongeza kwamba mechi ya Simba na Yanga ndiyo itatoa picha halisi ya ubingwa wa msimu huu, Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili waendelee kuwa kwenye mbio za ubingwa.

“Pointi tano ni nyingi kwa sababu ili uendelee kumfukuza mpinzani wako lazima uwe una shinda, game ambayo itatuonesha ubingwa ni ambayo tutakutana na Simba, lazima tushinde ili tuendelee kwa sababu hata Simba wana mechi ngumu pia”-Nadir Haroub, nahodha Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here