Home Kimataifa Rekodi mbovu Santiago Bernabeu, na mzimu wa Cr7 kuendelea kuwaumiza Juventus hii...

Rekodi mbovu Santiago Bernabeu, na mzimu wa Cr7 kuendelea kuwaumiza Juventus hii leo

8240
0
SHARE

Baada ya Cinema ya jana nchini Italia iliyowaacha watu midomo wazi pale Barca walipotupwa nje ya Champions League, leo Waitalia wengine watajaribu kuitikisa La Liga, ni Real Madrid vs Juventus.

Ni mchezo wa 21 kuwahi kuzikutanisha Real Madrid na Juventus unapigwa hii leo, kati ya mechi hizo ni mechi 20/21 zilikuwa za Champions League huku Madrid akishinda 10 na Juventus 8.

Juventus wana rekodi mbovu sana dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu, katika mechi zao 8 walizotembelea dimba hili Juventus walishinda michezo 2 tu wakasuluhu 1 na kupokea vipigo 5.

Ni mara moja tu kati ya 32 ndio Real Madrid walishindwa kufudhu katika hatua inayofuata ya mtoanao ya CL baada ya kushinda mechi ya kwanza ugenini na hii ilikuwa 1994/1995 baada ya kuifunga 3-2 Odense Boldklub ugenini na wakapigwa 2-0 nyumbani kwao.

Mchezo pekee ambao umechezwa mara nyingi kuliko Real Madrid na Juventus katika historia ya Champions League ni mchezo kati ya Real Madrid na Bayern Munich ambao hawa wameshakutana mara 24.

Wakati Juve wakiwa na clean sheets 6 katika mechi zao 10 za ugenini zilizopita ila tishio kubwa atakuwa CR7 ambaye katika mecho zote 6 alizokutana na Juve katika Champions League amefunga, akiwa amefunga jumla ya mabao 9.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here