Home Kimataifa Mwamuzi aisaidia Madrid kwenda nusu fainali, Bayern nao mambo safi

Mwamuzi aisaidia Madrid kwenda nusu fainali, Bayern nao mambo safi

9138
0
SHARE

Dalili za filamu iliyowatokea jana Barcelona zilianza kuonekana kama zinawatokea Real Madrid, hadi dakika ya 90 Juventus tayari walikuwa mbeleni kwa mabao 3 kwa 0 katika dimba la Santiago Bernabeu.

Shukrani kwa muamuzi Michael Oliver ambaye dakika ya 92 alitoa tuta kwa Real Madrid ambalo liliwapa bao ambalo liliitupa nje ya michuano ya Ulaya Juventus huku mlinda lango wao Gianluigi Buffon akipewa kadi nyekundu.

Bao la leo la Cristinao Ronaldo limeweka rekodu ya mchezaji mmoja kufunga mabao mengi dhidi ya mpinzani mmoja (10) akiivunja rekodi yake mwenyewe ya mabao 9 vs Bayern na Lionel Messi mabao 9 vs Arsenal.

Huko Allianz Arena Bayern Munich walisuluhu bao sifuri kwa sifuri na Sevilla, matokeo haya yanawafanya Barca kufudhu kwa aggregate ya bao 2-1 baada ya ushindi walioupata Hispania wiki iliyopita.

Kwa matokeo ya leo yanafanya nusu fainali kuwa na muwakilishi kutoka Italia, Ujerumani, Uingereza na Hispania, hii ikiwa mara ya kwanza kwa nusu fainali ya namna hiyo kutokea tangu mwaka 2010.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here