Home Kimataifa Takwimu zinazoitishia Barcelona wanapoelekea Roma leo

Takwimu zinazoitishia Barcelona wanapoelekea Roma leo

12939
0
SHARE

Ni timu mbili tu ambazo zilipindua matokeo ya mechi ya kwanza amabayo walifungwa 3-0, ni Deportivo La Coruna vs Ac Milan 2003/2004 na Barcelona vs PSG msimu uliopita, leo As Roma nao wanataka kufanya hivyo.

Lakini huu sio mtihani mdogo kwa As Roma kwani Barcelona wanaonekana kukamilika kila mahali, ukiacha eneo lao la ushambuliaji katika uzuiaji Barcelona hadi sasa wameruhusu mabao 3 tu, ikiwa ni idadi chache kuliko timu yoyote katika CL.

Utamu zaidi katika mechi hii ni uwezo wa As Roma katika uwanja wao wa nyumbani, katika mechi zao 5/6 wamefanikiwa kuwa na clean sheets huku wakishinda mechi zao 3 za mwisho dimbani hapo katika CL.

Katika mechi 4 za mwisho ambazo Barcelona wamecheza ugenini dhidi ya timu za Italia hawajashinda mchezo hata mmoja, Barca wamefungwa michezo 2 na kutoka suluhu michezo 2.

Lionel Messi pia hayuko vizuri anapokutana na timu za Italia haswa zikiwa katika ardhi yao ya nyumbani, katika mechi hizo 9  Messi amefunga mabao jumla ya mabao mawili tu tena yote dhidi ya Ac Milan.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here