Home Kitaifa Sababu 5 zinaisukuma Simba kutwaa ubingwa wa ligi 2017/18

Sababu 5 zinaisukuma Simba kutwaa ubingwa wa ligi 2017/18

14002
0
SHARE

Kama kuna kitu simba wanakihitaji kwa udi na uvumba bila shaka ni ubingwa wa ligi kuu tanzania bara. Simba inafanya kila namna kuhakikisha inashinda ubingwa wa ligi msimu huu na kuuondoa ukame wa misimu mitano bila ubingwa.

Kuna sababu nyingi za Simba kushinda ubingwa wa VPL msimu huu, lakini haimaanishi kwamba timu nyingine hususan yanga itakuwa ikiiangalia simba ikitwaa ubingwa kirahisi. Yanga imepitwa pointi sita na Simba lakini mabingwa watetezi wa ligi wana mchezo mmoja mkononi ambao watacheza dhidi ya singida united kwenye uwanja wa taifa.

Shaffihdauda.co.tz imeangalia sababu tano miongoni mwa nyingi ambazo zinaishukuma Simba kutwaa ubingwa wa ligi kama wataendelea kushinda mechi zao zilizobaki bila kuangalia matokeo ya timu nyingine.

Ubingwa VPL

Simba haijashinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara tangu walipofanya hivyo mara ya mwisho msimu wa 2011/12. Mpango pekee wa Simba kwa miaka ya hivi karibuni ni kushinda taji hilo ili kurejesha heshima Msimbazi.

Kimataifa

Mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu wamecheza mashindano ya Afrika msimu huu baada ya kukaa kwa misimu kadhaa bila kushiriki michuano ya Afrika ngazi ya vilabu. Kutolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika na kombe la Azam Sports Federation inamaanisha Simba isipochukua ubingwa wa ligi haitashiriki mashindano ya Afrika msimu ujao.

“Kushinda taji la ligi ndiyo itakuwa nafasi ya Simba kushiriki mashindano mengine ya kimataifa, bila kuchukua ubingwa wa ligi hatuwezi kuwa kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao na Simba haitabaki katika ukubwa wake nchini kama watu wanavyoijua”-John Bocco, nahodha wa Simba alizungumza baada ya kutolewa kwenye kombe la shirikisho Afrika.

Bilioni 1.3

Simba imetajwa kutumia zaidi ya bilioni 1.3 kufanya usajili wa baadhi ya nyota msimu huu. Haruna Niyonzima, Emanuel Okwi, Nicholas Gyn, John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni ni baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwa pesa nyingi ili kukifanya kikosi hicho kuwa imara zaidi kwa ajili ya mashindano mbalimbali.

Morali ya timu

Wachezaji wa Simba wameonesha morali ya juu kushinda ubingwa wa VPl msimu huu, nahodha wa Simba John Bocco akiongea baada ya timu yao kuondolewa kwenye mashindano ya kombe la shirikisho Afrika alisema: “Tutapambana kuhakikisha msimu huu tunakuwa mabingwa na itakuwa zawadi kwa mashabiki wetu, nawaomba mzidi kutuamini na kutupa sapoti. Tutapambana kwa jasho na nguvu zetu zote kuhakikisha msimu huu unakuwa wetu.”

Ubingwa kwa gharama yoyote

Simba ilitangaza bonus ya shilingi milioni 10 kwa wachezaji endapo watapata pointi tatu kwenye kila mchezo wa ligi. Kati ya hizo shilingi milioni 10, milioni tano wanachanga Simba headquarters na milioni tano nyingine anajitolea mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘Mo’.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here