Home Kitaifa Okwi anaziwinda rekodi za Kiiza na Tambwe VPL

Okwi anaziwinda rekodi za Kiiza na Tambwe VPL

9651
0
SHARE

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi amefunga goli lake la 17 la ligi kuu Tanzania bara msimu huu wakati Simba ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ushindi ambao unai unaiongezea Simba matumaini ya kushinda taji la VPL.

Okwi tayari ameshaivunja rekodi ya wafungaji bora wa msimu uliopita 2016/17 (Simon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Musa (Ruvu Shooting) ambao kila mmoja alifunga magoli 14 katika msimu huo. Okwi aliivunja rekodi hiyo Februari 26, 2018 baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo dhidi ya Mbao ambapo Simba ilishinda 5-0 ligi ikiwa mzunguko wa 19.

Kwa sasa Okwi anaifukuzia rekodi ya mganda mwenzake Hamis Kiiza ambaye alifunga magoli 19 msimu wa 2015/16 na kuwa mfungaji bora wa klabu ya Simba kwa msimuo. Rekodi nyingine anayoikimbiza ni ya Amis Tambwe mfungaji bora wa msimu wa 2015/16 ambaye alifunga magolki 21.

Okwi amebakiza magoli mawili kuifikia rekodi ya Kiiza ndani ya Simba huku akiwa anahitaji magoli matano ili kuivunja rekodi ya Tambwe mfungaji bora wa misimu wili iliyopita.

Simba imebakiza mechi nane za ligi ligi kuu, Okwi ana rekodi nzuri ya kufunga magoli mengi kwenye viwanja vya Dar (Uhuru na uwanja wa taifa) katika mechi nane ambazo zimebaki, Simba itacheza mechi tano nyumbani, kutokana na rekodi ya Okwi kwenye viwanja Dar huenda akazifikia rekodi hizo na kuzivunja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here