Home Kitaifa Majibu ya Mkwasa kuhusu tetesi Lwandamina ameondoka Yanga

Majibu ya Mkwasa kuhusu tetesi Lwandamina ameondoka Yanga

14793
0
SHARE

Taarifa inayo-trend kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni kuhusu kuondoka kwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga George Lwandamina, inadaiwa kocha huyo yupo Zambia na tayari klabu ya ZESCO imeshamtanga kuwa kocha wao mpya.

Taarifa ambayo inasadikiwa imetolewa na uongozi wa ZESCO United inaeleza kuwa Lwandamina ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kuchukua nafasi ya Tenant Chembo ambapo Aprili 8, 2018 alijiuzulu kuwa kocha wa muda.

Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema hajui lolote kuhusu taarifa hiyo, kama Lwandamina ameondoka basi hajamuaga.

“Mimi sijui chochote wala sina taarifa yoyote. Mimi najua yupo kama kaondoka mimi sijui kwa sababu hajaniaga”-Charles Boniface Mkwasa, Katibu Yanga.

Meneja wa timu ya Yanga Hafidh Saleh pia amesema hajui chochote na hawezi kuzungumzia suala la kocha.

“Mimi sijui lolote kuhusu hilo na siwezi kusema lolote kuhusu kocha. Muulize Katibu Mkuu maana yeye ndio msemaji”-Hafidh Saleh, meneja wa timu ya Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here