Home Kitaifa IMETHIBITISHWA: Lwandamina ameitosa Yanga

IMETHIBITISHWA: Lwandamina ameitosa Yanga

10484
0
SHARE

Imethibitika kwamba aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amerejea kwao Zambia na amejiunga rasmi la klabu yake ya zamani ZESCO United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kujiunga na Yanga.

Mwandishi wa habari za michezo nchini Zambia anayefahamika kwa jina la Sam amethibitisha kwamba klabu ya ZESCO imemtangaza rasmi Lwandamina kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo.

“Lwandamina ametangazwa rasmi kwamba amerejea ZESCO United leo. Baadhi ya mashabiki hawajafurahia kwa sababu wanamkubali sana kocha aliyeondoka (Tenant Chembo) ambaye alikuwa msaidizi wa Lwandamina. Baada ya Lwandamina kuondoka, Tenant Chembo aliendelea kubaki kama kocha wa muda kwa kipindi chote hicho.”

“Chembo ameamua kujiuzulu kwa sababu ZESCO iliendelea kumfanya kocha wa muda lakini baadaye alipata timu nyingine na kuamua kuachana na ZESCO.”

Novemba 25, 2016 Lwandamina alitambulishwa mbele ya waandishi wa habari kama kocha mkuu wa Yanga akichukua nafasi ya Hans van Pluijm. Ilielezwa Lwandamina alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here