Home Kimataifa Barcelona na Man City waoneshwa mlango wa kutokea Champions League

Barcelona na Man City waoneshwa mlango wa kutokea Champions League

9427
0
SHARE

Mo Salah aliweka rekodi ya mabao 8 ya Champions League kwa Liverpool ndani ya msimu mmoja, lakini dakika 28 baadae Firminho aliivunja baada ya yeye nae kufunga bao la 2 na la 8 msimu huu.

Liverpool wakaibuka kidedea cha mabao 1-2 dhidi ya Man City na sasa Jurgen Klopp anakuwa kocha wa kwanza kuwahi kumfunga Pep Gurdiola michezo 3 katika msimu mmoja wa ligi na hiki kikiwa kipigo cha 3 kwa City mfululizo.

Liverpool wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka nchini Uingereza kuwahi kufunga mabao 33 katika msimu mmoja wa CL, rekodi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Manchester United(32).

Habari kubwa ilikuwa nchini Italia ambapo As Roma wamefanya kile ambacho wengi hawakukitarajia baada ya kuitupa Barcelona nje ya michuano ya Champions League msimu huu, mara ya mwisho kwa Barca kupita katika hatua hii ilikuwa mwaka 2015.

As Roma wanakuwa timu ya 3 katika historia ya michuano ya Champions League kuwahi kupindua matokeo ya bao 3 katika mechi ya kwanza ambapo mwanzo timu mbili tu Deportivo la Coruna vs Ac Milan na Barcelona vs PSG walifanya hivyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here