Home Kitaifa Njombe Mji yajifariji

Njombe Mji yajifariji

6001
0
SHARE

Timu ya Njombe Mji imeendelea kufanya vibaya kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya kupoteza mechi yao ya ugenini kwa kufungwa 3-1 Stand United ya Shinyanga.

Stand United imeifunga Njombe Mji kwa mara ya pili mfululizo, Machi 30, 2018 Stand iliifunga Njombe Mji na kuitupa nje ya kombe la Azam Sports Federation Cup kabla ya Simba kuifunga tena Njombe Mji 2-0 kwenye mchezo wa VPL.

Afisa habari wa Njombe Mji Hassan Macho amesema bado timu yao itaendelea kupambana katika mechi saba zilizosalia ili kujihakikishia kubaki ligi kuu Tanzania bara.

“Bado tuna michezo saba ya ligi kuu, tumepoteza leo lakini sio kwamba tutapoteza michezo yote iliyobaki kwa hiyo tutapambana, matokeo yaliyotokea uwanjani hayatufanyi tushindwe kupambana katika michezo mingine”-Hassan Macho, afisa habari Njombe Mji.

“Timu ilikuwa na uchovu wa safasi pamoja na mabadiliko ya ratiba yaliyojitokeza hivi karibuni yalisababisha hata mipango ya mwalimu kukosa muunganiko. Mwalimu alijipanga kivingine lakini tumekuja kukutana na kitu kingine tofauti.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here